Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wenye nia ya kutaka kuwekeza kwenye sekta ya utalii nchini ili kuweza kutafsiri kwa vitendo maono ya Rais Samia kupitia filamu ya The Royal Tour

Ametoa kauli hiyo jana usiku Jijini Dare s Salaam wakati akizungumza na Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) kwenye mkutano wao wa mwaka ambapo kila mwaka hukutana mara moja kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali kuhusu ustawi wa Chama chao.

Amesema Serikali imepunguza ada ya kila mwaka kwa Mawakala wa Usafiri wa anga nchini ( TALA fee ) kutoka dola za Marekani 2,000 hadi dola 500

Pia ameeleza kuwa Serikali imejipanga kupunguza utitiri wa kodi katika sekta ya utalii ili kuhamasisha Wawekezaji zaidi katika sekta hiyo ili iweze kutoa ajira nyingi zaidi.

Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuwekeza miundombinu bora katika maeneo ya Hifadhi ikiwemo barabara zenye uwezo wa kupitika muda wote pamoja na usimikaji wa mtandao wa intaneti katika mlima Kilimanjaro.

Amesisitiza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi ili kuondoa vikwazo kwa wadau wenye nia ya kutaka kuwekeza hapa nchini.

Akizungumzia umahiri wa TASOTA, Waziri Chana amesema Wanachama hao wamekuwa wazalendo na Mabalozi wa kutangaza vivutio vya utalii nchini kwa wageni wanaotaka kuja kujionea uzuri wa Tanzania

” Najisikia fahari kuona TASOTA, wakifanya kazi usiku na mchana ya kuilinda na kuitetea taswira ya nchi kwa kuratibu na kupanga safari za watalii wanaotembelea Tanzania ”

Aidha, Dkt.Chana ameihaikikishia TASOTA kuwa yeye kama Waziri mwenye dhmama ataendelea kufanya kazi kwa ukaribu na jumuiya hiyo ili sekta ya utalii iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Naye Mwenyekiti wa TASOTA, Moustafa Khataw amesema anaishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao wa kutangaza uzuri wa Tanzania

” Tumekuwa tukifanya kazi zetu kwa weledi wa hali ya juu katika tasnia hii ya usafirishaji kwani ni biashara hii haina njia za mkato wala haina ujanja ujanja inahitaji watu wazalendo na wenye haiba nzuri katika kuwahudumia watalii wetu ” amesema Mwenyekiti Khataw.
Waziri  wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) Moustafa Khataw ikiwa ni kutambua mchango wake katika wa kuhakikisha Wanachama wa TASOTA wanafanya kazi zao katika mazingira wezeshi ikiwemo kero zao kutatuliwa kwa wakati


Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akizungumza na Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) kwenye mkutano wao wa mwaka ambapo amewapongeza kwa kuwa wazalendo wa kuilinda na kutetea nchi kwa watalii wanaoitembelea Tanzania

Mwenyekiti wa TASOTA, Moustafa Khataw akizungumza kabla hajamkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Dkt.Pindi Chana ambapo ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao wa kutangaza uzuri wa Tanzania

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana akikabidhiwa tuzo iliyotolewa na na Mwenyekiti wa Chama cha Mawakala wa usafiri wa anga Tanzania (TASOTA) Moustafa Khataw ikiwa ni kutambua mchango wake katika wa kuhakikisha Wanachama wa TASOTA wanafanya kazi zao katika mazingira wezeshi ikiwemo kero zao kutatuliwa kwa wakati

***********************

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...