Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana Februari 23, 2023 amefanya ziara katika Ofisi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mara ya kwanza tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo.
Mhe. Waziri Chana aliambatana na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Pauline Gekul, Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Dkt. Emmanuel Temu na Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma.
Hata hivyo Mhe. Waziri alipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya Wadau wa Sekta hizo ambao walinufaika na mikopo iliyotolewa na Mfuko huo hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...