Wizara ya Maliasili na Utalii imelaani vikali kufuatia matukio ya Askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu kuvamiwa na kuuawa na wananchi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao kisheria.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt.Pindi Chana ametoa kauli hiyo leo Jumatano Februari 2, 2022 Jijini Dodoma wakati alipokuwa akijibu hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii

Amesema kuanzia Machi mwaka jana hadi Februari mwaka huu jumla ya askari wa Uhifadhi na Watumishi 9 wameuawa huku jumla ya Askari wa Uhifadhi na Watumishi 68 wamejeruhiwa.

Amesema baadhi ya wananchi wanapokamatwa kwa makosa ya kuingia ndani ya hifadhi kinyume cha sheria kumekuwa na tabia ya wananchi kujipanga na kuvamia askari au kambi zao na kuwashambulia kwa silaha mbalimbali za jadi kama vile fimbo, sime, mapanga na mishale

Ameongeza kuwa matukio haya yamekuwa yakijrudia mara kwa mara katika maeneo mbalimbali hapa nchini na mara nyingi yamekuwa yakitokea pindi askari wa Jeshi la Uhifadhi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi

Amesema matukio haya yamepelekea askari wa Jeshi la Uhifadhi kujeruhiwa au kuuwawa pamoja na kusababisha uharibibifu wa mali za Serikali kama vile kuchoma moto magari, nyumba na vitendea kazi vingine muhimu kwa ajili ya shughuli za uhifadhi.

Katika hatua nyingine, Waziri Balozi Dkt. Chana amewataka wananchi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda rasilimali za Wanyamapori na Misitu hapa nchini na kuwataka wale wote wanaojichukulia sheria mkononi waache vitendo hivyo mara moja kwani ni kinyume cha sheria za nchi.

Aidha, Amesema Wizara kupitia Jeshi la Uhifadhi litaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama ili kukomesha vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuwabaini wale wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine ili sheria ichukue mkondo wake.




Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana alipokuwa akijibu hoja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika Bunge la Kumi na mbili leo Jijini Dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...