Njombe
Razack Urasa (33) mkazi wa mkoa wa Iringa amekamatwa na polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba gari No T 841 DMF aina ya Toyota ISIS mali ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabalang'anya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema mtuhumiwa ambaye alikuwa ni mlinzi wa nyumba ya mkurugenzi iliyopo mtaa wa Kambarage mjini Njombe amekamatwa akiwa na gari hiyo katika maeneo ya Kilolo mkoani Iringa.
"Gari hili lilipotea kabisa na hata mlinzi alipotea na katika uchunguzi wetu tukafanikiwa kulikamatia gari hili maeneo ya Iringa Kilolo na watuhumiwa tumewakamata ambao walikuwa ni walinzi wa nyumba husika,tunawaomba wananchi hawa walinzi mnaowaweka muwe mnayaamini makampuni yao"amesema Kamanda Issah
Sambamba na hilo kamanda wa polisi amebainisha kuwa jeshi hilo kwa kipindi kifupi limefanikiwa katika mambo mbali mbali kwenye wilaya zote za mkoa wa Njombe ikiwemo kuwakamata watu wawili katika kijiji cha Miva halmashauri ya mji wa Njombe kwa tuhuma ya kuuza mbolea feki.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...