Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam (DCC) imeishukuru Benki ya Biashara ya DCB
katika kusaidia uboreshaji wa elimu kwa kuchangia madawati 30 katika
shule ya msingi Kifuru iliyopo Kinyerezi, Ilala nje kidogo kutoka
katikati ya Jiji la Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa DCC Eng. Aman Mafuru amesema hayo katika hafla ya kukabidhi madawati
shuleni hapo ambapo amesema tayari serikali ipo katika mchakato wa
kuhakikisha shule zote za msingi zinazokabiliwa na changamoto ya
madawati zinapatiwa madawati hayo.
"Tutahakikisha
kwamba ushirikiano wetu na benki ya DCB Commercial Bank unasonga mbele
katika kuhakikisha kuwa tunatatua changamoto nyingi za huduma za kijamii
zinazoikabili manispaa na jamii kwa ujumla," alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori
Msaki, alisema katika jitihada za kuisaidia Serikali ya Tanzania
kuboresha sekta ya elimu nchini, benki ya Biashara ya DCB ina mpango wa
kuchangia angalau madawati 1,000 katika shule mbalimbali za msingi
nchini kati ya mwaka 2023/2025.
Msaki
alisema madawati 30 yanayotolewa katika Shule ya Msingi Kifuru iliyopo
Kinyerezi, Ilala, Dar es Salaam ni miongoni mwa madawati 150 ambayo
benki hiyo itasaidia shule mbalimbali za msingi za Manispaa ya jiji
hilo.
Alisema pamoja na
kuboresha sekta ya elimu, madawati hayo pia yatahakikisha wanafunzi
wanasoma katika mazingira mazuri, hivyo kusaidia kuboresha ufaulu wa
wanafunzi katika shule za sekondari.
"Tunaunga
mkono kampeni yetu iliyopewa jina la 'Elimu Mpango mzima na Mama Samia'
inayotambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya taifa," alisema.
Msaki
alisema kupitia Bodi ya wakurugenzi ya Benki ya DCB inayoongozwa na Bi
Zawadia Nanyaro inalenga kuhakikisha kuwa wanafunzi wa shule za msingi
wanakuwa na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Alisema
benki hiyo pia inaunga mkono mipango ya manispaa katika kuboresha sekta
ya elimu mkoani humo na nchi nzima kwa ujumla ambapo katika hafla hiyo
benki inakabidhi madawati 30 kati ya 150 yaliyopangwa kukabidhiwa kwa
halmashauri za manispaa ya Dar es Salaam.
"Tunaamini
serikali kupitia kwa Rais Samia Suluhu Hassan inafanya kazi kubwa
kuboresha sekta ya elimu, lakini serikali pekee haiwezi kumudu gharama
zote za elimu kwa wanafunzi nchini," alisema.
Alisema
benki hiyo itaendelea kusaidia mipango mbalimbali ya maendeleo ya
serikali katika sekta ya elimu katika shule hiyo inayokabiliwa na
changamoto lukuki ikiwemo majengo ya madarasa, vyoo, madawati pamoja
na huduma nyingine za kijamii katika shule hiyo na nchi nzima kwa
ujumla.
.Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru (
kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki
(kulia), Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo ( wa pili kushoto)
na Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga wakishangilia baada ya Benki ya DCB
kukabidhi msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru ikiwa ni
sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima
na Mama Samia” ,shuleni hapo, Kinyerezi, nje kidogo kutoka katikati ya
Jiji la Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru ( kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki wakikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru yaliyotolewa na DCB ikiwa ni sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Elimu kata ya Bonyokwa, Sylvia Lyimo, Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga, Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo na Mkuu wa Shule ya Kifuru, Wilfred Lwagaza.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru
akizungumza kabla hajapokea msaada wa madawati 30 yaliyotolewa na Benki
YA DCB, shuleni hapo, Kinyerezi, Dar es Salaam leo.
Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru ( kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori Msaki wakikata utepe kuashiria makabidhiano ya msaada wa madawati 30 kwa shule ya msingi Kifuru yaliyotolewa na DCB ikiwa ni sehemu ya kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini leo. Wengine kutoka kushoto ni Ofisa Elimu kata ya Bonyokwa, Sylvia Lyimo, Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga, Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo na Mkuu wa Shule ya Kifuru, Wilfred Lwagaza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori
Msaki akishikana mikono na wanafunzi wa shule ya msingi Kifuru baada
ya kuwakabidhi msaada wa madawati 30 kama sehemu ya kampeni yake
inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima na Mama Samia” jijini
leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Isidori
Msaki akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa madawati 30
kwa shule ya msingi Kifuru shuleni hapo, Kinyerezi nje kidogo kutoka
katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo.
Diwani wa Kata ya Bonyokwa, Tumika Malilo akizungumza katika hafla hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Biashara ya
DCB, Rahma Ngassa akipiga picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya
msingi Kifuru mara baada ya hafla hiyo, shuleni hapo leo. DCB
ilikabidhi msaada wa madawati 30 yakipokewa na Kaimu Mkurugenzi wa
Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi Amani Mafuru.
Mkuu wa Shule ya Msingi Kifuru akitoa neno la shukrani
baada ya Benki ya Biashara ya DCB kukabidhi madawati 30 kwa shule yake
kupitia kampeni yake inayoendelea ya elimu iitwayo “Elimu Mpango Mzima
na Mama Samia”. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Isidori
Msaki, Ofisa Elimu wa jiji, Spora Tenga, Diwani wa Kata ya Bonyokwa,
Tumika Malilo na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Mhandisi
Amani Mafuru.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...