Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini ,Georgia Mutagahywa (wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na Katibu wa afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Lilian Mwanga baada ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya matibabu vilivyotolewa na Barrick katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na hospitali ya Mwananyamala. Siku ya wanawake duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
Meneja Mawasiliano wa Barrick nchini, Georgia Mutagahywa (wa tatu kushoto) akimkabidhi vifaa vya hospitali kwa Daktari wa hospitali ya Mwananyamala Eliyafie Huruma sehemu ya vifaa, vilivyotolewa na kampuni ya Barrick katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Wengine pichani ni wafanyakazi wa Barrick na hospitali ya Mwananyamala.Siku ya wanawake duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka.
KATIKA kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Wafanyakazi Wanawake wa kampuni ya Barrick kutoka ofisi ya Dar es Salaam wametembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala na kukabidhi vifaa mbalimbali vya kusaidia matibabu vilivyotolewana kampuni hiyo.
Pia wafanyakazi hao wamepata fursa ya kutembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo.
Akiongea na uongozi wa Hospitali hiyo leo Machi 7, 2023 Meneja Mawasiliano wa Barrick Nchini (Corporate Communications and Country Liasion Manager) Georgia Mutagahywa, amesema katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu, pamoja na kampuni kuwa na programu mbalimbali za ndani pia imeandaa programu za kusaidia jamii .
Amesema Barrick, imekuwa ikitoa kipaumbele kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha sekta ya afya nchini ambapo kupitia fedha za uwajibikaji kwa jamii imeweza kujenga vituo vya afya katika maeneo yanayozunguka migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara.
Kwa upande wake, Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo, Lilian Mwanga. ameishukuru Barrick kwa msaada huo sambamba na baadhi ya wafanyakazi wake kujitolea muda wao kutembelea hospitali na kutembelea wagonjwa walioalazwa hospitalini hapo ikiwemo Wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi..
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...