Benki ya Exim Tanzania imezindua akaunti maalum kwa ajili ya wanawake ijulikanayo kwa jina la ‘Supa Woman’ ikilenga kusogeza karibu na kuhamasisha huduma za kibenki kwa kundi hilo muhimu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella ameipongeza hatua hiyo kwa kuwa inakwenda sambamba na dhamira ya serikali ya katika kuwakwamua kiuchumi wanawake nchini.
Hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo iliongozwa na RC Mongella jijini Arusha hii leo wakati akifungua Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa ulioandaliwa na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) kwa kushirikiana Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) ukilenga kukuza ushiriki wa wanawake na vijana katika Biashara.
Akizungumzia huduma hiyo Bw Mongella alisema inakwenda sambamba na wito wa serikali unaozihimiza taasisi za kifedha nchini kubuni huduma mbalimbali zinazolenga kuwasaidia wajasirimali na wafanyabiashara wadogo hususani vijana na wakina mama kujikwamua kiuchumi.
“Ni faraja kwetu serikali kuona kwamba taasisi za kifedha nchini zinaendelea kuitikia wito unaotolewa kila siku na viongozi wetu waandamizi akiwemo Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu ambae amekuwa akizihimiza taasisi za kifedha nchini kuwa karibu zaidi na makundi haya hususani wakina mama na vijana.’’
“Ujio wa akaunti hii ya Supa Woman ni mrejesho sahihi wa wito huo wa serikali…nawapongeza sana benki ya Exim nawasihi sana walengwa waichangamkie,’’ alisema RC Mongella.
Benki ya Exim ni moja ya wadhamini wakubwa wa maonesho hayo.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi wa Bodi ya Exim Tanzania Bi Irene Mlola alisema pamoja na kuwapongeza waandaaji wa mkutano huo alisema tukio hilo limetoa fursa kwa benki hiyo kukutana na wadau wake muhimu kwa kuwa wao kama benki wanaamini uwezeshaji wa wanawake na ujasiriamali unasalia kuwa nguzo muhimu za mipango ya maendeleo ya kiuchumi.
“Exim tunaamini uwezeshaji halisi unaweza kupatikana tu kwa kuwekeza katika ustawi wa wanawake. Ujasiriamali, na hasa ujasiriamali wa wanawake na vijana barani Afrika, unazidi kutazamwa kama hoja ya msingi katika ukuaji wa uchumi kwa ujumla katika bara hili na hiyo ndio sababu Exim tumekuja na huduma hii ya Supa Woman tukilenga kuunga mkono mtazamo huo.’’ Alisema
Zaidi akizungumzia huduma hiyo Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda alisema inalenga kurahisisha uendeshwaji wa biashara miongoni mwa wafanyabiashara wanawake nchini kwa kuwawezesha kuweka akiba kwa urahisi, kupokea malipo kwa njia za kidijitali sambamba na kuliunganisha kundi hilo na fursa mbalimbali za kibiashara ikiwemo mikopo.
“Pamoja na dhamira yetu ya dhati ya kuwa karibu zaidi na wanawake, huduma hii mpya ni muitikio wa maoni ambayo tumekuwa tukiyapokea kutoka kwa wadau wetu mbalimbali wakiwemo wateja wetu wanawake ambao kiukweli wana ndoto kubwa za mafanikio kwenye shughuli zao hivyo na sisi tukaona tuna jukumu la kwenda nao sambamba katika kufanikisha malengo yao,’’ alisema.
Awali akizungumzia Mkutano na maonyesho hayo ya siku sita Ofisa Mtendaji Mkuu wa TAWEN, Bi Florence Masunga alisema ukiwa na kauli mbiu “Strengthening African Women and Youth Businesses For a Sustainable Tomorrow” mkutano huo unalenga kukuza ushiriki wa wanawake na vijana katika Biashara.
“Pamoja na kuipongeza serikali kwa namna inavyozidi kufungua fursa mbalimbali kwa wanawake na vijana nchini naiomba iweke mkazo zaidi katika kushughulikia changamoto ya vikwazo vitokanavyo na urasimu kwenye mipaka baina ya mataifa jirani kwa kuwa vinarudisha nyuma jitihada za wanawake na vijana kujiendeleza kiuchumi.’’ alisema
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella (wa tano kulia) akitangaza uzinduzi rasmi wa akaunti maalum kwa ajili ya wanawake wajasiriamali ijulikanayo kwa jina la ‘Supa Woman’ ya benki ya Exim Tanzania inayolenga kusogeza karibu na kuhamasisha huduma za kibenki kwa kundi hilo muhimu.Hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo umefanyika jijini Arusha hii leo kwenye Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa. Wengine ni pamoja na viongozi waandamizi wa Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN), Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania wakiwahudumia wateja mbalimbali waliotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lililopo kwenye Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Afrika yanayofanyika jijini Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella (wa pili kulia) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi wa Bodi ya Exim Tanzania Bi Irene Mlola alipotembelea banda la maonesho ya huduma za benki hiyo lililopo kwenye Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa yanayofanyika jijini Arusha. Wengine ni pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) Bi Florence Masunga (kulia) pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella akizungumza na washiriki wa Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa yanayofanyika jijini Arusha ulioandaliwa na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) kwa kushirikiana Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) ukilenga kukuza ushiriki wa wanawake na vijana katika Biashara.
Mkurugenzi wa Bodi ya Exim Tanzania Bi Irene Mlola akizungumza na washiriki wa Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa yanayofanyika jijini Arusha ulioandaliwa na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) kwa kushirikiana Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) ukilenga kukuza ushiriki wa wanawake na vijana katika Biashara. Benki ya Exim ni moja ya wadhamini wakubwa wa maonesho hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw John Mongella (wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini wa Maonesho na Mkutano wa pili wa wanawake na vijana wafanyabiashara barani Africa yanayofanyika jijini Arusha ulioandaliwa na Mtandao wa Uwezeshaji Wanawake Tanzania (TAWEN) kwa kushirikiana Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC) ukilenga kukuza ushiriki wa wanawake na vijana katika Biashara. Benki ya Exim ni moja ya wadhamini wakubwa wa maonesho hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...