Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias
akishuhudia mteja Dosian Augustine akifanya muamala katika mashine ya
ATM ya Tawi la Mlimani City mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya
uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inayolenga kuwapa
watumiaji wa ATM za NBC nafasi ya kujishindia Zawadi na kuweza kuwa
sehemu ya kufurahia Udhamini wa Benki ya NBC kwenye Ligi Kuu ya Tanzania
Bara.
Meneja wa Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Lilian Mutalemwa akitoa
zawadi ya Jezi kwa mmoja wa washindi wa Kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA
ATM ZA NBC Dosian Augustine baada ya kushinda alipofanya muamala wake
katika mashine ya ATM Mapema leo.
Meneja wa Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Lilian Mutalemwa akitoa
zawadi ya mpira kwa mmoja wa washindi wa Kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA
ATM ZA NBC Bi Rehema Mushi baada ya kushinda alipofanya muamala wake
katika mashine ya ATM Mapema leo.
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya NBC na wateja mara baada ya
uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC katika hafla
iliyofanyika mapema leo katika Tawi la Mlimani city [/caption] Dar es
Salaam.Machi 24,2023- Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza
uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inayolenga kuwapa
watumiaji wa ATM za NBC nafasi ya kujishindia Zawadi na kuweza kuwa
sehemu ya kufurahia Udhamini wa Benki ya NBC kwenye Ligi Kuu ya Tanzania
Bara. Zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia
mechi za Ligi kuu ya Mabingwa ya NBC, jezi, na zawadi nyingine kemkem.
Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC Bw, David Raymond, akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya uzinduzi wa
kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC zilzofanyika mapema leo katika
tawi la Mlimani city.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika katika Tawi Benki la NBC la Mlimani City, Mkuu wa kitengo cha masoko wa NBC Bw, David Raymond, alisema, Kampeni hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC inalenga kuhamasisha wateja wa NBC na wasio wateja wa NBC kutumia mashine za ATM za NBC kufanya miamala yao.
Wateja ambao watatumia kadi zao za ATM kufanya miamala mbalimbali katika kipindi cha kampeni watapata nafasi ya kushinda zawadi za kusisimua, ikiwa ni pamoja na tiketi za kushuhudia Ligi ya Mabingwa ya NBC, Jezi, na zawadi nyingine kemkem. "Tunayo furaha kuzindua kampeni hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC ambayo inawazawadia watumiaji wote wa ATM za NBC ikiwa ni wateja wa NBC na wasio wateja wa NBC.
Tunaelewa umuhimu wa urahisi katika huduma za benki, tunazidi kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi na wateja kwa kuongeza ATM mpya kwenye maeneo mbali mbali nchini. Watumiaji wa ATM za NBC wanaweza kuweka pesa kwenye akaunti yoyote ya NBC kupitia ATM zilizopo kwenye matawi yetu nchi nzima.
Alisema David
Aliongeza “Pia wale wasiokuwa na akaunti yoyote wanaotumiwa fedha kwa
kutumia huduma ya NBC Cash Popote, wanaweza kutoa pesa hizo kwenye ATM
yoyote ya NBC. Wote walio na kadi za VISA, Union Pay na Mastercard
wanaweza kutumia ATM za NBC kutoa pesa. Makundi yote haya yanayo nafasi
sawa ya kujishindia Zawadi hizi katika kampeni hii. Tunaamini kuwa
watumiaji wa ATM za NBC wataendelea kufurahia huduma zetu,
tunawakaribisha wote watumie ATM za NBC."
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias.
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) katika hafla ya
uzinduzi wa kampeni ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC zilzofanyika
mapema leo katika tawi la Mlimani city.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidijitali wa Benki ya NBC, Ulrik Tobias aliongeza kuwa zawadi hizo zitakuwa ni za papo kwa papo, pale mteja akifanya muamala wake kwa kutumia ATM ya NBC atapata kujua kuwa ameshinda zawadi gani kwa kuangalia nyuma ya risiti ya muamala wake.
“Sisi kama benki ya NBC, daima tunawaweka wateja wetu karibu na kuhakikisha wanafurahia huduma zetu wakati wowote na popote. Kampeni yetu ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC Tunafurahi kuwapa wateja wetu nafasi ya kushinda tiketi za kuona Ligi ya Mabingwa, jezi, na vitu vingine vya kumbukumbu ya Ligi ya NBC. Tunatumai kuwa kampeni hii itaimarisha zaidi uhusiano wetu na wateja wetu pamoja na watumiaji wote wa ATM zetu.
"
alisema Urlik Kampeni hii inawalenga watumiaji wote wa ATM za Benki ya
NBC za Dar es Salaam na Kibaha. Kila mtumiaji wa ATM za NBC akishafanya
muamala, achukue risiti yake, aigeuze nyuma kuangalia zawadi
aliyoshinda. Kisha aende na risiti yake kwenye tawi lolote lililo karibu
naye ili kuchukua zawadi yake. Tukio hili lilihudhuriwa na wateja wa
NBC na wanahabari ambao walipata fursa ya kujifunza zaidi kuhusu kampeni
hii ya MKEKA WA USHINDI NA ATM ZA NBC na kuzungumza na wafanyakazi wa
NBC.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...