NA MWANDISHI WETU, KIBAHA

MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaj Aboubakar Kunenge amehimiza ushirikiano baina ya Taasisi za Umma, Binafsi na watendaji kwenye Halmashauri ili kazi ya kuwatumikia wananchi iwe rahisi.

Ameyasema hayo wakati akifungua semina ya kujenga uelewa wa shughuli za taasisi mbalimbali za umma na binafsi ikiwemo Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT) na watendaji kutoka Halmashauri za Mkoa wa Pwani Machi 30, 2023.

 GBT ni taasisi ya Kiserikali ambayo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango ikisimamiwa na Msajili wa Hazina. (TR).

 Alisema wataalamu lazima wajue viongozi wa kisiasa hawawezi kuwa na maamuzi mazuri kama wataalamu hawajafanya kazi ya kitaalamu inavyotakiwa.

 “Serikali ni moja, mlipaji ni mmoja, fedha inatoka fungu moja na inavyopatikana iwe ni Halmashauri au Bodi ya Michezo ya kubahatisha yote inaingia sehemu moja kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha au PST.” Alisema na kuongeza ….

 Haiwezekani kwenye Halmashauri kukawa na watendaji kutoka kila taasisi ya serikali na kushauri ili utendaji wa taasisi hizo kwenye maeneo ambayo ni vigumu kwa watendaji wao kuwepo ili kuwatumikia wananchi ni vema kukawepo na makubaliano yatakayowezesha utendaji kazi ukawa rahisi bilaya vikwazo, alifafanua Alhaj Kunenge ambaye alifuatana na Wakuu wote wa wilaya za Mkoa huo.

 “Kama tuna majukumu ambayo tunawea kufanya kwa niaba ya wenzetu mnaweza kukasimu shughuli zenu na zikafanywa na watu wa Halmashauri, lazima tufanye kwani serikali ni moja.” Alisema.

 Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bw. James Mbalwe alisema Bodi imefika Mkoani humo kwa lengo la kujitambulisha rasmi kwa watendaji wa Mkoa ili kuongeza ufahamu wa kamati, uwepo wa taasisi na kuongeza ufahamu juu ya usimamizi na uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini.

 Pia kuimarisha ushirikiano katika usimamizi na udhibiti wa sekta na kuomba kamati ya Ulinz na Usalama ya Mkoa kushirikiana na GBT ili kudhibiti wavunjaji wa sheria ya michezo ya kubahatisha hapa mkoa wa Pwani, alisema Bw. Mbalwe.

Alisema wanaona umuhimu wa kutoa elimu mara kwa mara kwa vile GBT ni taasisi change iliyoanza mwaka 2003

 Alisema semina kama hizo zimekuwa na manufaa makubwa katika kurahisisha utendaji wa GBT na kutolea mfano Mkoani Kigoma.

“Kazi yetu ni udhibiti, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa michezo ya kubahatisha nchini na haifanyi biashara na iko chini ya Wizara ya Fedha chini ya Msajili wa Hazina.” Alifafanua

 Bw. Mbalwe alimeelezakuimarisha ushirikiano katika usimamizi wa sekta na hivyo tunaomba kamati ya usalama ya mkoa kuongeza ushirikianoz aidi katika kudhibiti wavunja sharia ya Michezo ya Kubahatisha.

“Nina sisitiza Michezo ya Kubahatisha ni Burudani na sio Ajira au njia ya kujitafutia kipato.” Alifafanua Bw. Mbalwe.

Kuanzishwa kwa GBT kumewezesha sekta ya michezo ya kubahatisha kuratinbiwa vizuri zaidi na iweze kuchangia ipasavyo katika pato la taifa na wananchi wanaojishughulisha kwenye michezo hiyo wanalindwa ipasavyo.

 “Sekta inakuwa kwa kasi na kwa sababu hiyo kunahitaji uratibu makini ili iendelee kukua katika namna ambayo utaratibu unaopasa bila kupoteza malengo ya msingi ya kuanzishwa kwake.” Alifafanua Bw. Mbalwe.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge akifungua semina hiyo kwenye Mji wa Kibaha Machi 30, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bw. James Mbalwe akizunguzma kwenye semina hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine kutoka Halmashauri za Mkoa huo
Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Huduma za (DCS) Bw. Daniel Ole Sumayan (katikati) na Mkurugenzi wa Ukaguzi na Matekelezo Bw. Sadick Elimsu
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa GBT, Bw. James Mbalwe (wapili kushoto) Mkurugenzi wa Masuala ya Shirika, Bw. Daniel Ole Sumayan (wakwanza kushoto). Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Bw. Rashid Mchatta.

Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...