KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameiagizaa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupeleka fedha haraka kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kinambeu iliyopo Iramba mkoani Singida.
Ujenzi wa Zahanati hiyo umekwama kwa zaidi ya miaka 10 hali ambayo imeendelea kusababisha changamoto na adha kubwa Kwa wananchi katika kupata huduma za afya na hivyo kulazimika kutembea umbali mrefu.Katibu Mkuu Chongolo ametoa maelekezo hayo kwa TAMISEMI baada ya kupokea taatifa ya ujenzi wa Zahanati hiyo ulianza mwaka 2011 lakini hadi sasa haijakamilika.
Chongolo alifika kwenye Zahanati hiyo Kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi na majengo yaliyopo lakini kutokana na hali aliyoona amelazimika kutoa maelezo hayo kwa TAMISEMI .
"Naiagiza TAMISEMI na Halmashuri ya Iramba kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika haraka iwezekanavyo ili wananchi waondokane na adha ya kukosa huduma za afya."
Zahanati hiyo ujenzi wake hadi sasa umegharimu Sh.Milioni 185.9 ambapo Mhisani kutoka Japan alitoa Sh. Milioni 158.8, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Sh.Milioni 20.04 na jamii kutoa nguvu kazi zenye gharama ya Sh.Milioni 7.06 na mkandarasi aliishia kukamilisha kazi ya ujenzi wa kuta na kupaua Desemba mwaka 2015.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...