Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
WANAWAKE kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar es Salaam wameshiriki katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani, leo tarehe 8 Machi 2023 yaliyofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Akizungumza na Michuzi Blog, Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Coretha Komba amesema kupitia Kaulimbiu ya ‘Ubunifu na Mabadiliko ya Teknolojia, Chachu katika kuleta usawa wa Kijinsia’, amesema kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya teknolojia yamesaidia kuleta usawa wa kijinsia.
“Kwa sasa baada ya mabadiliko ya Teknolojia, Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kufanya vitu ambavyo walikuwa wanafanya Wanaume pekee,” amesema Dkt. Coretha.
Dkt. Coretha amesema wamejifunza mengi katika Maadhimisho ya mwaka huu, lakini pia wamepata fursa ya kutoa misaada katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Wanawake kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Ndaki ya Dar Es Salaam wakiwa kwenye maandamano kwenye siku ya Wanawake duniani katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanawake hao wa Chuo Kikuu cha Mzumbe wameongozwa na Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Coretha Komba
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...