Wanawake katika Manispaa ya Singida wameaswa kujenga utamaduni wa kuwa marafiki na watoto wao, ili kuzikabili changamoto mbalimbali, ikiwemo ukatili wa kijinsia, ubakaji na ndoa za utotoni.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo,Mstahiki meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Maulid Kiaratu, amesema hayo Mach, 08, 2023, kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, katika kiwanja cha Bombadia.
Mstahiki Meya amesema kuwa, kwa kujenga urafiki na watoto wao, wazazi watabaini changamoto nyingi, zinazowakabili kundi hilo, na hivyo kuzipatia ufumbuzi wa haraka, kabla ya madhara zaidi.
“Sasa Wanawake, kidogo tumeanza kusahau malezi ya watoto wetu, tukijenga utamaduni wa kuwa rafiki wa watoto, watakueleza matatizo yao, wapi ameshindwa, na nani kafanya nini...”, amesema Kiaratu.
Pamoja na malezi bora, Mstahiki Meya amefafanua kuwa, hivi sasa serikali imeweka mazingira nafuu yanayowezesha mwanamke anapata haki.
Ameongeza kuwa, serikali imewapa uwezo wa kisheria wanawake kupitia usaidizi wa kisheria katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo akatoa wito kujitokeza zaidi, ili wapate haki itakayowaweka huru.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Singida mjini, Lucia Mwiru, amewaomba wanawake kuendeleza tabia ya kupendana, badala ya kupigana majungu, jambo linalohatarisha umoja wao.
Amesema kuwa, panapokuwa na umoja, amani na upendo, daima panakuwa na mshikamano mkubwa, baina ya kundi hilo muhimu katika familia na jamii kwa ujumla.
“Wanawake tuheshimiane, wanawake tupendane, kila mtu amheshimu mwenzie kulingana na nafasi aliyonayo, lakini mwanamke mzuri na kiongozi mzuri ni Yule anayejishusha kwa wenzake,”amesema Lucia.
Baadhi ya Wanawake walioshiriki maadhimisho hayo, akiwemo Anna Laswai na Veronica Timotheo, wamesema siku hiyo ni muhimu kwao na katika manispaa ya Singida, yanawaweka pamoja bila kujali anatoka sehemu gani, yanaimarisha uhusiano, na wanashiriki maonyesho mbalimbali ya ujasiriamali, hivyo kuwafanya wakue kifikra.
Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa march nane kila mwaka, kwa lengo la kuhamasisha na kukuza maendeleo yao kisiasa, kijamii na kiuchumi, pia kuendeleza harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na waume.
Mgeni rasmi , Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida , Mhe. Yagi Maulid Kiaratu, akishiriki katika maandamano ya wanawake wa Manipsaa ya Singida kuelekea katika eneo la Buraudani tayari kwa kupanda miti ili kuboresha mazingira ya eneo hilo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Yagi Kiaratu, akipanda mti katika eneo la Bustani la Burudani baada ya kupokea maandamo ya wanawake wa Manispaa ya Singida, wakiwemo wajasiriamali na wanawake kutoka taasisi mbalimbali ndani ya Manispaa ya Singida
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akipokea maandamano ya wanawake waliokuwa wakipita mbele yake katika uwanja wa Bombadia, Manispaa ya Singida. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Lucia Mwiru, na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo Mama Shomari
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida akipokea maandamano ya wanawake waliokuwa wakipita mbele yake katika uwanja wa Bombadia, Manispaa ya Singida. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Singida Mjini Lucia Mwiru, na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho hayo Mama Shomari
Wanawake kutoka taasisi mbalimbali wameshiriki Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani. Pichani ni wanawake kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida wakiwa katika picha ya pamoja
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida, Bi. Upendo Naftali, akitambulisha wageni katika maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia, Manispaa ya Singida
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akiambatana na wageni Meza kuu kukagua mabada ya maonesho ya wajasiriamali katika Manispaa ya Singida. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Kulanga Matia Kanyanga pamoja na Diwani viti Maalum Saidath Mziray
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Yagi Kiaratu akiambatana na wageni Meza kuu kukagua mabada ya maonesho ya wajasiriamali katika Manispaa ya Singida. Pamoja nae ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Kulanga Matia Kanyanga pamoja na Diwani viti Maalum Saidath Mziray
Kikundi cha ngoma ya kabila la Kinyaturu kikitoa burudani mbele ya mgeni rasmi ( Pichani hayupo) wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani, Manispaa ya Singida
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...