Njombe

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ameagiza halmashauri za wilaya hiyo kuongeza kiwango cha fedha za mikopo ya asilimia 10 inayotolewa bila riba kwa vijana wanawake na watu wenye ulemavu ili iwe na tija zaidi kwa wanufaika ikiwemo ujenzi wa viwanda vya matunda ya Parachichi.

Kasongwa ametoa agizo hilo wakati akifungua kongamano la wajasariamali kata ya Njombe mjini ambapo amesema ni wakati wa halmashauri kutoa mikopo mkubwa itayowawezesha wajasiriamali kuanzisha miradi mikubwa kama vile viwanda vya parachichi madawati ili waweze kujikwamua kiuchumi.

“Tunauwezo wa kuanzisha viwanda, tuna malighafi nyingi ambazo zinatupwa kwa mfano siku za nyuma tuliona zilimwagwa Parachichi tani kumi tano kwa hiyo mikopo itolewe mikubwa na yenye tija ili watu waweze kufanya vitu ambavyo vina maana”Amesema Kissa Kasongwa DC Njombe

Aidha Kissa ameagiza halmashauri kutoa muda wa kutosha Kwa halmashauri kabla wajasiriamali kuanza kurejesha mikopo yao kwa kumekuwa na taratibu ya kutoa muda mchache kwa wajasiriamali kurejesha mikopo yao.

Vile vile amesema halmashauri ya wilaya ya Njombe inatarajia kukuza uchumi wa halmashauri hiyo na vipato vya wananchi kwa kuanzisha misitu ya matunda aina Parachichi zao ambao limeendelea kukua kwa kasi katika mkoa wa Njombe.

"Kuna kijiji kinaitwa Ikang'asi ambacho kina eneo la ekari 89,000 sisi tumeamua eneo hili liwe Msitu wa Parachichi ambao baadhi ya eneo tutatoa kwenye mradi wa kitaifa wa BBT ambao Mh.Rais amezindua Dodoma,sasa niwaombe vikundi vya Vijana kuchangamkia fursa"Kissa Kasongwa DC wa Njombe.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...