MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) waendelea kuadhimisha siku ya Wanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8 kwa kuandaa wanawake waliofanikiwa kukaa na Wasichana na wanawake pekee kuelezea historia zao na jinsi walivyofanikiwa.

Ikiwa ni namna moja ya kuhamasisha wasichana kufikia malengo yao huku wakijua kuwa wanawake ambao walipitia changamoto mbalimbali na kufikia malengo yao.

Akizungumza katika Nafasi Salama ‘Safe Space’ iliyoandaliwa na TGNP jijini Dar es Salaam Machi 24, 2023, mwanamke ambaye ameanzisha Kampuni ya Masuala ya TEHAMA, Asha Abinallah amewaaswa Wanawake na Wasichana kutokutumia mitandao ya kijamii kuweka picha ambazo hazina maadili kwani picha hizo zinaweza kutafsiri huyu ni mwanamke wa namna gani na kupoteza nafasi ya kazi.

Pia ameomba kutumia mitandao ya kijamii kujiingizia kipato na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuweza kupambania faida zilizopo mitandaoni nakutoitumia kwa kufanya vitu misivyo na faida kwao.

Akitoa historia yake mpaka alipofikia wakati wa ‘Safe Space’ ya wasichana na wanawake amesema kuwa lengo ni kuwahamasisha wanawake na wasichana kuto kukata tamaa pale wanapodhamiria kufanya jambo fulani.

Asha akiwahamasisha wanawake na wasichana katika nafasi salama amesema kuwa ujasiri bila kuangalia nani anasema nini ndio umemletea mafanikio makubwa ya kutembea nchi mbalimbali na kupata tuzo za umahili katika TEHAMA.

Amesema kuwa safari yake ya kujitambua yeye ni nani ilianza akiwa na miaka 30, hivyo amewahamasisha wasichana katika umri wao kujitambua na kuanza kufanya mapinduzi katika malengo yao ya maendeleo.

Pia amewahamasisha vijana na wasichana kufanya kazi kwa bidii pale wanapopata nafasi ya kufanya kazi ili waweze kufikia malengo.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP), Liliani Liundi wakati akifungua nafasi Salama kwa wasichana na wanawake amesema kuwa wamekuwa wakiandaa nafasi salama kwa wasichana na wanawake ili kujifunza mambo mbalimbali tangu mwaka 1999.

Amesema kunawanawake wengi wamefanikiwa katika mambo mbalimbali hiyo TGNP watakuwa wanamchukua mmoja mmoja ili kuweza kuelezea safari zao za maisha ili wasichana waweze kujifunza kutoka kwao licha ya changamoto zilizopo.

Lilian amesema kwa TGNP ‘KE storia’ zitaweza kuwahamasisha wanawake na wasichana kufanya makubwa bila kuwa na woga wowote uliopo ndani yao kwa kusikiliza storia za waliofanikiwa.

“Nitoe rai kwa wanawake, wasichana na wananchi wote wa Tanzania kuendelea kujifunza matumizi sahihi ya teknolojia kuliletea manufaa na maendeleo taifa badala ya kutumia teknolojia, hasa mitandao ya kijamii kufanya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia.” Amesema Lilian

Pia amewahamasisha kutumia teknolojia ili kuelimisha jamii kuachana na vitendo hivyo na kuchukua hatua ili kutokomeza vitendo hivyo.


Mwanamke aliyefungua Kampuni ya Masuala ya TEHAMA, Asha Abinallah akizngumza na wasichana na wanawake katika Sehemu Salama kwa Wasichana na Wanawake iliyofanyika Machi 24, 2023 katika Ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijinsia Tanzania(TGNP), Liliani Liundi akizungumza wakati wa kufungua Sehemu Salama kwa wasichana na wanawake iliyofanyika Machi 24, 2023 jijini Dar es Salaam.
Burudani ikiendelea.






Matukio Mbalimbali wakati wa KE stori ya Mwanamke aliyefungua Kampuni ya Masuala ya TEHAMA jijini Dar es Salaam Machi 24, 2023.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...