Na. Damian Kunambi Njombe.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewaomba viongozi wa dini wilayani humo kusimamia nafasi zao za kutoa huduma za kiroho na kiimani sanjari na kuiombea wilaya hiyo na taifa kwa ujumla ili kuzidi kuwa na amani, upendo na maendeleo.

Mwanziva ameyasema hayo alipofanya kikao na viongozi hao ofisini kwake kilicholenga kutambuana, kujenga umoja na ushirikiano na kuongeza kuwa viongozi wa dini wanaposimama na kuliombea taifa kunasaidia kuleta anani na maendeleo kwa Taifa.

"Viongozi wa dini mna nafasi kubwa sana katika kuleta amani kwa nchi na wilaya yetu, mnapomuombea Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kunamsaidia kutekeleza vyema majukumu yake ya kuliongoza Taifa la Tanzania, vilevile kwa viongozi wa wilaya yetu hivyo niwaombe sana kutukumbuka katika maombi".

Aidha viongozi hao wameonyesha kufurahishwa na kikao hicho ambacho kimeonyesha wazi kuwa wana umuhimu na mchango kwa taifa hivyo wameahidi kuendeleza zaidi utaratibu walionao wa kuliombea Taifa, Wilaya pamoja na viongozi wake.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...