Na Rahma Khamis Maelezo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduk Dkt Hussein Ali Mwinyi amevitaka vyombo vya habari vya nje na ndani ya Nchi kutumia lugha ya Kiswahili na kuiimarisha lugha hiyo ili iendelee kutumika duniani kote.

Hayo ameyasema katika Ukumbi wa Sheikh Idriss Abul-Wakikil kikwajuni wakati alipokua akifungua kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani.

Amesema lugha ya kiswahil ni lugha ya Taifa ambayo inatumika katika shughuli mbalimbali hivyo ipo haja kwa vyombo vya habari kuitumia ipasavyo katika matamshi yake kwani kufanya hivyo kunapelekea kuikukuza lugha hiyo.

Aidha amefahamisha kuwa taaluma itakayopatikana katika kongamano hilo itawasaidia wanahabari nguli na chipukizi kuhamasisha kutumia lugha hiyo katika jamiii na kuiendeleza.

Katika hatua nyengine Dkt. Mwinyi amewataka wataalamu wa lugha ya Kiswahili pamoja na waandishi wa habari kuendelea kutumia fursa kutoka nje ya nchi kwa lengo la kukikuza Kiswahili.

Hata hivyo Dkt. Mwinyi amewapongeza wale wote walioshirikiana kwa pamoja katika kufanikisha kongamano hilo na kuwataka wageni kutembelea vivutio vya utalii kwalengo la kuitangaza lugha ya Kiswahili kwa wengine ili lugha hiyo iendelee kuenea zaidi.

Nae Waziri wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amewataka waandishi wa habari kushirikiana na Baraza la Kiswahili kuweza kupata tafsiri za maneno ili kufanyakazi zao kwa ufanisi zaidi.

Aidha amefahamisha kuwa Wizara inaendelea kuiendeleza lugha hiyo ingawa kuna baadhi ya changamoto zinajitokeza kutokana na utandawazi ambao unapelekea kukichafua kiswahii jambo ambalo linarejesha nyuma jitihada hizo.

Kwa upande wake Mwenyekiti Baraza la Kiswahili Saade Said Mbarouk amsema jambo la kufurahisha kuona Idhaa za Kiswahili zinatumia lugha hiyo kwani zimesaidia kukuza na kukieneza kwa kasi duniani.

Aidha amezishauri idhaa zinazotumia lugha hiyo, waandishi wa habari na jamii kwa ujumla kuendelea kuitumia hata wakiwa katika mataifa ya nje.

Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo Lugha ya Kiswahili katika utangazaji na atharizake, Fursa na changamoto za mawasiliano ya habari katika maendeleo ya Kiswahili na Changamoto za matumizi ya Kiswahili katika kazi ya utangazaji ndani ya vituo vya kazi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu “KISWAHILI NI NYENZO YA MAWASILIANO TUJIAMINI KITUMIA.”
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe Dkt.Huseein Ali Mwinyi  akipokea zawadi kutoka kwa Mtunzi wa Vitabu Rizik Juma Mohammed wakati alipotembelea banda  la maonesho la  KITABU KILA MAHALA nje ya Ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul-Wakil wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Idhaa za Kiswahihili Huko kikwajuni Mjini Zanzibar. Machi 18 2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka Afisa mauzo kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota Lilian Christian kuhusiana na Vitabu wanavyouza wakati alipokuwa akitembelea maonesho yaliyokua nje ya Ukumbi uliofanyika Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Huko Kikwajuni Mjini Zanzibar. Machi 18 2023.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Afisa masoko wa kampuni ya uchapaji vitabu  (E$D) Tumsifu Usiri  kuhusiana na vitabu wanavyochapisha wakati alipokuwa akitembelea maonesho yaliyokua nje ya Ukumbi uliofanyika Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Huko Kikwajuni Mjini Zanzibar. Machi 18 2023.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...