TIMU za Friends of Tulia Trust (Wanawake na Wanaume) zimeondolewa kwenye mashindano ya Sodo 4 Climate ya Betika yanayoendelea katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam.
Katika mashindano hayo timu ya Friends of Tulia Trust imetupwa nje ya mashindano na timu ya Espanyol kwa kipigo cha mabao 2-0 kwa upande wa wanaume sanjari na timu ya Wanawake kufungwa mabao 2-1 dhidi ya hao hao, Espanyol.
Mashindano hayo yana lengo mahsusi kuikumbusha jamii umuhimu wa kutunza mazingira yanaendelea katika viwanja hivyo vya Coco Beach, Dar es Salaam huku kila siku ya Jumamosi miche mbalimbali inapigwa kwenye viwanja hivyo.
“Mashindano haya yanahamasisha kutunza mazingira na tayari tumetoa vifaa, elimu ili kutunza Bahari sanjari na kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yamekuwa ni tatizo kubwa duniani kote,” amesema
Sodo 4 Climate ni mashindano ambayo yanachezwa kwa Mpira maalum wa kufuma. Kaulimbiu ya mashindano hayo ni ‘Shabiki Soka, Sio uharibifu wa Mazingira’, mashindano yanachezwa kwa mfumo wa mtoano (Knock Out).
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...