Washiri wa Kongamano hilo wakiwa katika picha ya pamoja

Na Byarugaba Innocent,Kibaha
HALMASHAURI ya Mji Kibaha leo tarehe 1 Machi,2023 imeendesha semina ya kuwajengea uwezo maafisa Elimu kata,walimu walimu wa shule za msingi na sekondari juu ya masuala ya VVU/UKIMWI mahala pa kazi kwa lengo la kuondoa unyanyapaa na ukatili wa kijinsia.

Siwema Cheru ni Mratibu wa UKIMWI wa Halmashauri ya Mji Kibaha amesema semina hiyo ni mwendelezo wa Mafunzo mengine ambayo yamekuwa yakitolewa kwa wadau mbalimbali ili kuondoa vitendo vya unyanyasaji sehemu za kazi na kwamba sasa wamefikiwa waratibu wa Elimu kata na walimu ambao ni wadau wakubwa kwenye jamii na wanakaa na wanafunzi muda mrefu ambao pia ni wahanga.

Dr.Mariam Ngaja ameeleza kuwa walimu wakipata uelewa wa semina hiyo wanawajibu wa kuwafundisha wanafunzi wao kuhusu afya ya uzazi kwa Vijana na maradhi yanayoambukizwa kwa njia ya ngono na Elimu ya madawa ya kulevya.

Ngaja ameongeza kuwa semina hiyo ambayo ni utekezaji wa Kawaida wa Idara ni utekelezaji wa mkakati wa nne wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI Tanzania hasa kwa wasichana balehe na wanawake Vijana.

Mwalimu Augustine Seso aliyeshiriki semina hiyo ameishukuru Halmashauri kwa kuigharamia na kwamba imewafikia muda muafaka na Sasa wanakwenda kwenye jamii kutimiza lengo la kutoe Elimu ili kuondosha unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwenye jamii.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...