Na Jane Edward, Arusha

Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa Rais Muungano na mazingira Dr Suleiman Jafo amekitaka kiwanda kinacho tengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo (AtoZ)ambao wamekuwa wakilalamikiwa kila wakati kutokana na changamoto ya utiririshaji maji machafu kwenye makazi ya wananchi huenda kilio hicho kikamalizika baada ya kukamilika mtambo wa kuchuja maji machafu ya kiwanda hicho.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha AtoZ na kukagua mradi wa mitambo mikubwa ya kuchujia maji pamoja na kuridhishwa na mitambo hiyo ambayo inalenga kumaliza malalamiko ya wakazi wa eneo hilo .

"Nawaelekeza viongozi wa kiwanda hiki kuwa uwepo wa mitambo hii hakuna sababu tena ya kusikia malalamiko yeyote kwa wananchi juu ya utiririshaji wa maji machafu "Alisema Waziri Jafo

Amefafanua kuwa wizara yake haitakuwa tayari kuunga mkono kuona wananchi wanalalamika juu ya kadhia hiyo na kwamba lazima sheria na taratibu zifuatwe ili kuepuka malalamiko hayo.

"Serikali inatambua jitihada nzuri na uwekezaji mliouweka hapa nchini lakini tuangalie na afya za wakazi wanaozunguka kiwanda hiki"Alisema

Kwa upande wake meneja wa baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kanda ya kaskazini Lewis Nzali alisema wamekuwa wakifanya vipimo vya maji hayo na mara nyingi yamekuwa yakikidhi vigezo vinavyokubalika.

Amesema kutokana na maagizo ya Waziri watakuwa kila mara wakifanya ukaguzi na kupima maji hayo kwa mustakabali wa wananchi wa eneo hilo.

Naye Afisa usalama na Mazingira kutoka kiwanda hicho cha AtoZ Harryson Rwehumbiza amesema maji yote yanayo tiririshwa kuelekea kwenye makazi hayo yamekuwa salama na yamekuwa yakitumika katika shughuli mbalimbali ikiwemo bustani.

Vilevile ameahidi mbele ya Waziri kuwa maji yanayotoka kiwandani kuwa na viwango vinavyokubalika kwa matumizi kwani kiwanda hicho kimefanya uwekezaji mkubwa ili kuhakikisha hakiwi kero kwa wananchi wanao wazunguka.

Waziri Dr Jafo akikagua mitambo ya maji katika kiwanda cha nguo AtoZ.
Waziri Dr Jafo akitoa maelekezo ya serikali katika kiwanda cha nguo AtoZ jijini Arusha.

Eng Harryson Rwehumbiza afisa Afya na mazingira kiwanda cha nguo AtoZ akifafanua jambo kwa waandishi.
Mhandisi Rwehumbiza akielezea moja ya mitambo ya kupitisha maji hayo.
Meneja wa baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kanda ya kaskazini akizungumza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...