Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi
Ndugu Daniel Chongolo amesema Tanzania haina mzigo mkubwa wa Madeni kama
ilivyo kwa mataifa mengine ya Afrika Mashariki, huku akiwashangaa watu
wanaobeza mpango wa Serikali kukopa Fedha Nje ya Nchi.
Chongolo
ameyazungumza hayo leo Machi 01, 2023 wakati wa kikao cha shina namba 6
Katika kata ya Ulemo, Wilaya ya Iramba ikiwa ni Siku ya Tatu ya Ziara
yake mkoani Singida.
" Hatua ya Serikali kukopa ni kuendelea
Kuijenga Tanzania ili iwe imara Kiuchumi kama ilivyo kwa mataifa
yaliyopiga hatua Kimaendeleo",alibainisha Chongolo.
Amesema yapo
mafanikio mengi ya kiuchumi ikiwemo sekta ya Elimu na Miundombinu
ambayo serikali ilikopa zamani na imeshamaliza kulipa, lakini hadi
sasa Watanzania wanaendelea kufaidika
Chongolo ametoa rai kwa
Jamii kuacha maneno ya watu ambao haiwatakii mema nchi yetu,amesema nchi
yetu inakopa na nchi nyigine zote zinazotuzunguka zinakopa, na nchi
myingine zote duniani zinakopa zinapokuwa na masuala mahususi ambayo
wanadhani kwa kupata fedha na kuyatekeleza yana tija kwa wananchi wake.
Kwa Upande wake Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sophia Mjema, amewaasa
viongozi wa Chama hicho katika ngazi zote, kuendelea kueneza Sera za
CCM kwa Vitendo ikiwa ni pamoja na kuweza kuisemea na kuisimamia Miradi
inayofanywa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dkt
Samia Suluhu Hassan.
Katibu mkuu wa CCM Ndugu Danie Chongolo
ameambatana na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi
Ndugu Sophia Mjema na Katibu na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa
Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Iramba Ndugu Mwigulu Mchemba (kushoto) wakati wa kikao cha wanachama wa CCM wa shina namba 6, Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Uramba, katikati ni Mwenyekiti wa shina hilo Ndugu Evangelina Petro Samuel.
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...