Na Mwandishi wetu Jeshi la Polisi
Askari wa Jeshi la Polisi kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) wamewafariji mahabusu na wafungwa kwa kuongea nao na kuwapa vitu mbalimbali katika Gereza la Segerea lengo likiwa ni kutambua kundi hilo muhimu kwa taifa.
Akiongea na waandishi wahabari leo marchi 10 2023 mwenyekiti wa mtaandao wa Polisi wanawake kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam mrakibu mwandamizi wa Polisi SSP-ANITHA SEMWANO amesema wanatambua umuhimu wa kundi hilo katika jamii ambapo amesema wao kama Jeshi la Polisi walitumia siku ya wanawake duniani kuwapa elimu ya ukalii wa kijinsia na namna ya kutoa taarifa za ukalii katika jamii.
Aidha SSP Mwano amesema kundi hilo lipo gerezani hapo kwa mujibu wa sheria na kusema kwamba wao walikinzana na sheria za Nchi na kupelekea kuwa katika mazingira hayo.
Ameeleza kuwa Jeshi hilo linatambua mchango mkubwa kundi hilo ambapo amebainisha kuwa kwa kutambua hilo wakufunzi wa chuo hicho Pamoja na wanafunzi wa kozi ya uofisa na mkaguzi msaidizi wa Polisi waliona vyema kuungana na kutoa mchango huo kwa wafungwa waliopo katika gereza hilo.
Nae mrakibu wa Magereza SP IYUNGE SAGANDA amesema mchango wa askari hao utakuwa msaada mkubwa kwa wafungwa hususani wafungwa kike ambapo ametoa wito majeshi na taasisi nyingine kuiga mfano mzuri wa Jeshi la Polisi kwa kumbuka makundi ya wahitaji.
Sambamba na hilo mwanafunzi wa kozi ya mkaguzi msadizi wa Polisi WP GIFT MSOWOYA amesema kuwa wao wanatambua pia umuhimu wa kundi hilo mara ambapo amebainisha kuwa wafungwa hao watakapomaliza kifungo chao watakwenda kulitumikia taifa na kuongeza mchango wa maendeleo katika Nchi yetu.
Kwa upande kwa mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam ambae ndiye mlezi wa mtaandao wa Polisi wanawake TPFNET kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Daktari Lazaro Mambosasa amewapongeza askari hao kwa moyo wao wa kipeke wa kujali makundi maaalum.
Mambosasa pia ametoa wito kwa mtandao huo kuangalia makundi mengine yenye uhitaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...