Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) alipokutana kwa ajili ya mazungumzo na Viongozi wa Benki ya Dunia Jijini Washington DC, Marekani, hivi karibuni.
Viongozi wa Benki ya Dunia aliokutana nao ni Bi. Mari Pangetsu, Mkurugenzi Mtendaji wa Sera ya Maendeleo na Ushirikiano wa Benki ya Dunia, na Bi. Mamta Murthi, Makamu wa Rais wa Maendeleo ya Watu katika Benki ya Dunia.
Kutoka GPE Mwenyekiti wa Bodi Dr. Jakaya Kikwete aliambana na Bi. Laura Frigenti, Mtendaji Mkuu wa GPE na Bw. Charles North, Naibu Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.
Mkutano huo ulilenga katika kuboresha ushirikiano uliopo kati ya GPE na Benki ya Dunia katika kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wa kike na wa kiume katika nchi zinazoendelea.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...