Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambayo inaadhimishwa kila Machi 8 kila mwaka leo Machi 5 Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo kimefanya Kongamano ikiwa ni kuendeleza harakati za Ukombozi wa mwanamke kwani kwa namna ya kipekee wanajumuika na wanawake na wanaharakati kote duniani kusherekea mafanikio yaliyofikiwa, kutafakari changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni ubunifu na mabadiliko ya teknolojia, chachu ya kuleta usawa wa kijinsia. Kupitia kauli mbiu hii inatukumbusha kuona umuhimu wa ujumuishi wa wanawake katika masuala ya teknolojia. Kwa upande mwingine, inatukumbusha kufanya tafakuru juu ya namna teknolojia ni kichocheo au kizuizi cha kujileta usawa wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo SGT. Habiba Seif Kiibegeya kutoka Dawati la Jinsia na Watoto kituo cha Polisi cha Urafiki amesema Teknolojia hapa nchini imekuja kwa kasi sana bila kujua nini maana ya Teknolojia pamoja na watu wengine hawaelewi matumizi mazuri ya masuala hayo ya Teknolojia.
Amesema watanzania wengi wanaadhirika na Teknolojia hasa hizi simu za mkononi kwani kuna watu wanazitumia kwa matumizi mabaya ambapo jeshi la polisi linapata kesi nyingi sana zinazohusiana na Simu za Mkononi ambapo watu wengine wanajipiga picha za utupu na kuzituma mitandaoni bila kujua kama zitakuja kuwaletea matatizo huko mbeleni kwani picha hizo zinaishi.
Pia amewaasa wanawake pale wanapopata Simu wazitumie kwa manufaa hasa kwenye kuwaingizia kipato ili kuona umuhimu wa Teknolojia kama inavyoeleza kwenye kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani tofauti na hivyo zitakuja kuleta matatizo makubwa kwa vizazi vijavyo.
“Wanawake wenzagu tukemee ukatili wa kijinsia, usione mwanamke mwenzako au mtoto wa jirani anafanyiwa ukatili ukakaa kimya kwa kutokuchukua hatua yoyote ya kuripoti kwenye vyombo vya usalama kwa kuogopa kuharibu mahusiano mazuri na jirani yako maana kufanya hivyo na wewe utakuwa ni miongoni mwa wale wanaofanya ukatili wa kijinsia” Alisema SGT Kiibegeya
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Liundi amesema Uongozi wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Mabibo kinabidi ukutane na uongozi wa wa Mtandao huo ili kuangalia ni kwanamna gani wanaweza kupanga mikakati na kuona ni kwanamna gani inaweza kwenda mbele kwa kasi kwani inaonekana kuna kazi wanawake hawazipi kiupaumbele mpaka zinachukuliwa na wanaume.
Pia amesema mabadiriko ya Teknolojia yapo na yataendelea kuwepo hivyo inabidi wanawake kujipanga ipasavyo ili kuendana na mabadiliko hayo maana wasipofanya hivyo wataachwa nyuma na fulsa zinazokuja zitaendelea kuongeza pengo la Kijinsia zaidi kama juhudi za haraka hazitafanyika.
“Ni lazima masuala ya kipato yazungumziwe kila sehemu kwasabau Teknolojia ina gharama na kama suala la uchumi halitashughulikiwa ikiwa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi basi wananchi wa hali ya chini hasa wanawake hawatoweza kuendana na Teknolojia inavyokwenda .” alisema Liundi
Akisoma risala kwa mgeni rasmi Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Mabibo Neema Mwinyi amesema takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa asilimia 22 ya wafanyakazi kwenye fani ya Aritifisho Inteligent kuwa ni wanawake. Lakini, pia inaonesha kuwa asilima 73 ya waandishi wa habari kwenye nchi 125 wamekutana na ukatili wa kijinsia mtandaoni wakiwa katika kazi yao.
Pia amesema maendeleo ya Teknolojia pia yameleta pengo kubwa la kimtandao duniani kwa asilimia 10 ambapo ni asilimia 48 tu ya wanawake wanaofikiwa na kutumia mitandao ukilinganisha na asilimia 58 ya wanaume. Nchini Tanzania takwimu zinaonesha kuwa ni asilimia 35 tu ya wanawake wanatumia simu za mikononi.
“Maadhimisho haya leo na kwa mwezi huu mzima, yanatupa fursa ya kujadili na kuja na mikakati mdhubuti itakayotusaidia kutumia Teknolojia na ubunifu ili kutatua changamoto zinazowakabili wanawake na makundi mengine ya pembezoni, ikiwemo changamoto zinaotokana na Teknolojia yenyewe ili kuweza kuwa kichocheo cha kutokomeza ukatili wa kijinsia na usawa wa kijinsia kwa ujumla wake.” Alisema Mwinyi
SGT. Habiba Seif Kiibegeya kutoka Dawati la Jinsia na Watoto kituo cha Polisi cha Urafiki akizungumza wakati wa kufungua kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP).
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP).
Mwenyekiti wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Mabibo Neema Mwinyi akisoma risala kwa mgrni rasmi SGT. Habiba Seif Kiibegeya kutoka Dawati la Jinsia na Watoto kituo cha Polisi cha Urafiki wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililoandaliwa na Kituo cha taarifa na Maarifa cha Mabibo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani yatakayofikia kilele Machi 08, 2023.
Mgeni rasmi SGT. Habiba Seif Kiibegeya kutoka Dawati la Jinsia na Watoto kituo cha Polisi cha Urafiki(wa tatu kushoto) akikabidhiwa risala na Mwenyekiti wa Kituo cha taarifa na Maarifa cha Mabibo Neema Mwinyi mara baada ya kusoma risala hiyo kwenye kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Habari na Mawasiliano wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Monica John akitoa mrejesho wa kongamano la maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Kituo cha Taarifa na Maarifa Mabibo kwa kushirikiana na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe mbalimbali
Picha za pamoja
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...