Na Karama Kenyunko Michuzi TV
Mahakama ya hakimu Mkazi kisutu imemuachia huru mfanyabiashara Amani Filipo (38) aliyekuwa akikabiliwa na tuma za kumuua askari wa Kikosi Cha Usalama Barabarani, Sajenti Mensah kwa kumpiga risasi kufuatia upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yake.
Filipo anadaiwa kumuua Sajenti Mensah kwa kumpiga risasi baada ya kumvamia katika kibanda cha polisi cha kupumzikia kilichopo mataa ya Sayansi kwa lengo la kutaka kupora.
Hukumu hiyo imesomwa leo March 20, 2023 mahakamani hapo na Hakimu Mkazi Mkuu Romuli Mbuya aliyekasimiwa mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mbuya amesema, hakuna shahidi yeyote kati ya mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi walioweza kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa Filipo ndio aliua.
"Upande wa mashtaka ulileta mashahidi sita na vielezo sita ikiwemo taarifa ya daktari aliyefanyia uchunguzi mwili wa marehemu na ramani ya tukio lakini upande wa mashtaka wameshindwa kuthibitisha shtaka hilo kwani ushahidi wao ulikuwa na matobo mengi" amesema Hakimu Mbuya.
Akichambua ushahidi wa baadhi ya mashahidi, Hakimu Mbuya amesema, ushahidi wa shahidi wa kwanza ambaye alikuwa ni askari aliyekuwepo eneo la tukio uliegemea katika utambuzi wa kuona kwa macho eneo la tukio
Amesema, tukio hilo lilitokea usiku wa saa mbili mazingira yalikuwa magumu kwani tukio lilitokea muda mfupi sana inadaiwa mazingira yalikuwa ya kuogopesha huku ushahidi wa mwanga wa taa ukiww na mkanganyiko ambapo alitaja mianga saba ambazo ni mwanga wa barabarani, mbaramwezi, majumbani, taa za barabarani huku maelezo ya polisi yakitaja umeme wa uzio wa TTCL na taa za barabarani.
"Aidha ushahidi wa utambuzi wa mshtakiwa haukuzingatia kwani maelezo hayakutolewa polisi na ushahidi wa gralide la utambuzi umeonekana hauna thamani kwani kanuni za ushahidi hazikuzingatiwa na mtoa taarifa za mshtakiwa hakuletwa Mahakamani kutoa ushahidi
"Mshtakiwa alikamatwa na mtoa taarifa ambaye alikuwa akimfahamu hadi jina lake upande wa mashitaka wameshindwa kumleta Mahakamani kutoa ushahidi, hivyo mahakama imeona mshitakiwa hana hatia na ninamwachia huru," ameongeza.
Aidha akichambua ushahidi wa Daktari, hakimu Mbuya amsema Daktari katika uchunguzi wake aligundua kuwa marehemu katika eneo la kifua chake upande wa kulia mbavu zilivunjika na mapafu yalitoboka na jeraha lilikuwa na urefu wa setimeta tatu, hivyo marehemu alipoteza damu nyingi.
Alisema katika ushahidi huo, upande wa mashitaka wameshindwa kuthibitisha shtaka hilo kwani ushahidi ulikuwa na matobo mengi, hivyo Mahakama imeona hana hatia inamwachia huru.
Marehemu Sajenti Mensah ambaye alikuwa ni askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, alipigwa risasi Julai 22, mwaka 2016, eneo la Sayansi, Kijitonyama, Dar es Sallaam saa mbili usiku,
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo mareheu akiwa na askari mwenzake wakitoka katika kibanda cha polisi cha mapumziko, baada ya kumaliza zamu yao walianza safari ya kwenda nyumbani gafra walisikia sauti ya mtu nyuma yao akiwaamuru kwamba simameni na mtoe vitu vyote mlivyonavyo
Marehemu Sajenti Mensah ambaye alikuwa ni askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, alipigwa risasi Julai 22, mwaka 2016, eneo la Sayansi, Kijitonyama, Dar es Sallaam saa mbili usiku,
Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa Mahakamani hapo mareheu akiwa na askari mwenzake wakitoka katika kibanda cha polisi cha mapumziko, baada ya kumaliza zamu yao walianza safari ya kwenda nyumbani gafra walisikia sauti ya mtu nyuma yao akiwaamuru kwamba simameni na mtoe vitu vyote mlivyonavyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...