Katika maadhimisho hayo ya wiki ya maji yalio fanyika leo katika Kata ya Ayamohe-Mbulu Mjini,na kuratibiwa na Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira (MBUWASA),Wananchi na viongozi wameshiriki kupanda miti katika vyanzo vya maji ili kuendelea kuvitunza na kuvilinda vyanzo hivyo.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James,ameeleza mafanikio makubwa yaliofikiwa ktk kuboresha,kusogeza na kuimarisha mfumo wa huduma wa upatikanaji maji katika wilaya ya Mbulu.Aidha Komred Kheri James ameeleza dhamira ya Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kuendelea kujenga miradi mikubwa ya maji na kuhakikisha kuwa maji yanawafikia wananchi wote ktk maeneo ya mjini na vijijini ili kurahisisha huduma na kukuza uchumi wa wananchi.
Pamoja na mambo mengine Komred Kheri James amesisitiza umuhimu wa kutunza na kulinda vyanzo vya maji,pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wote ambao shughuli au vitendo vyao vina athiri uwepo wa vyanzo vya maji.
Katika maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya amejumuika pamoja na Kamati ya usalama,watumishi,viongozi na wananchi katika zoezi la kupanda miti ili kuendelea kuvitunza na kuviendeleza vyanzo vya maji.
Wiki hii ya maji kwa wilaya ya Mbulu,imeendelea kutumika kama fursa ya kupata taarifa juu ya maendeleo ya sekta ya Maji,kubaini changamoto,kukutanisha wadau wa maji,kueleza mafanikio ya sekta ya maji,na kuwashirikisha wananchi katika mipango ijayo ya mageuzi makubwa katika utoaji na upatikanaji wa huduma ya maji.
Mkuu wa wilaya amewapongeza watumishi na viongozi wa sekta ya maji kwa kazi kubwa na nzuri,na amewaomba wananchi waendelee kuipa ushirikiano (MBUWASA)ili iendelee kufanya vyema zaidi.
#KwaPamoja,tunaijenga Mbulu Yetu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...