Njombe

Polisi mkoani Njombe imetoa tahadhari kwa wafanyabiashara na wakulima wanaobeba hela nyingi mikononi wakati wa kuzipeleka benk au kukabidhiana baada ya kuuza mazao na kuomba kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama ili vitoe huduma ya polisi ya kusindikiza kwa ajili ya usalama.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah ameeleza hayo wakati akizungumza na kutoa elimu kwa madereva wa malori pamoja na Madalali katika kituo cha magari ya mizigo kilichopo Edina halmashauri ya mji wa Njombe.

"Msikubali kubeba hela kwenye mifuko na siku ukiwa umebeba hela njoo tuambie kuwa nimebeba hela mimi nitakupa askari hiyo ruhusa ipo kuna sheria unachukua askari akusindikize,nyie njooni na hata wakati mnawapa wakulima hela askari atakuwepo"amesema Kamanda Issah.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...