Muunguzi wa Wodi ya watoto kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bi. Asteria Henjewele akifafanua jambo kwa wafanyakazi baada ya kutembelea na kuwafariji wazazi na watoto waliolazwa katika hospitali hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia Ndaki ya Dar es Salaam Bi Victoria Mnyanyi akitoa utambulisho Kaimu Mkuu wa Ndaki Dkt Coretha Komba na wanajuiya wa chuo kikuu Mzumbe  kwa maafisa ustawi wa jamii hospitali ya Taifa ya Muhimbili.



Mkuu wa Idara ya  Ustawi wa Jamii Bw. Daniel Mutani akiwashukuru wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam kwa mchango wa matibabu walioutoa ilikusaidia matibabu ya watoto.
Kaimu  Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Coretha Komba  akiongea  kabla ya kukabidhi mchango wa matibabu.


Wafanyakazi wa Chuo kikuu Mzumbe na maafisa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili katika Picha ya pamoja.

WANAJUMUIYA ya Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya watoto na kutoa msaada kwa kuchangia matibabu yenye thamani ya shilingi 1,580,000/= kwa watoto waliolazwa katika hospitali hiyo ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofikia kilele  Machi 8, 2023.

Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo leo  Machi 7,  2023, Kaimu Mkuu wa Ndaki hiyo, Dkt. Coretha Komba anamshukuru Mungu ambaye amewajalia uzima wanajumuiya ya Chuo Kikuu Mzumbe na kuweza kufika katika hospitali hiyo kuweza kuwapa msaada wa matibabu watoto ambao wanauhitaji.

“Sisi tumekuja pia Ili tujifunze, kama kauli mbiu yetu inavyosema; 'Tujifunze Kwa Maendeleo Ya Watu'. tunaamini leo ni mwanzo wa kuendelea kushirikiana ili tuweze kuwasaidia hawa watoto kwa maendeleo yao na Taifa. Hivyo tutaendelea kuja na kutoa misaada pale inapohitajika”.Amesema Dkt. Komba

Akipokea msaada huo, Afisa Ustawi wa Jamii Bi. Ester Mwambogoja amewashukuru wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kwa kuchangia matibabu na amewaomba wafanyakazi hao kutokuishia hapo. Pia amewakaribisha kufika hospitalini kwa ajili ya kuwajulia hali wagonjwa mbalimbali mara wapatapo nafasi kwani inawapa faraja.

Aidha, mmoja wa wahadhiri wa Chuo hicho, Dkt. Godbertha Kinyondo ameshauri Hospitali ya Muhimbili kushirikiana na vyuo kikiwemo Chuo Kikuu Mzumbe kwani wanachuo hasa wanaosomea Shahada ya uzamili (Masters) hufanya tafiti zinazolenga changamoto mbalimbali za jamii. Hivyo, hospitali inaweza kushirikiana na Chuo ili kuweza kupata mada za kufanya utafiti zinazohusiana na aina fulani ya changamotoza za mazingira wanayotoka wagonjwa na kufanya utafiti utakaotoa majibu na mbinu za kipambana na maradhi hayo.

Naye Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Bw Daniel Mutani amekishukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa mchango waliochangia matibabu kwa watoto waliopo wodini lakini amesema kuna watoto na wagonjwa wengine wanatibiwa matibabu ya nje hawapo wodini kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu, tunaomba muendelea kuwasaidia wagonjwa hao pia.

"Tunawashukuru wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuchangia matibabu ya watoto. Lakini pia nawaomba msichoke muendelee na moyo wa kujitoa kwani kuna wagonjwa wa nje wanahitaji msaada wa matibabu, naomba mtu yoyote au kikundi kuja kuwasaidia kwa uhitaji ni mkubwa”.. Amesitiza

Pia tunaupokea Ushauri kuhusu kushirikisha wanafunzi katika kufanya tafiti tutaufikisha kwenye ngazi husika, kiukweli ni ushauri mzuri kwani ingawa kuna tafiti za kitabibu, lakini zipo zingine zinagusa jamii moja Kwa moja." Alisema Bw. Mutani

Awali muuguzi wa Wodi ya watoto wenye saratani Esteria Henjewele amesisitiza wazazi na walezi kuwafanyia ukaguzi wa afya ya mara kwa mara watoto ili iwapo watagundulika na tatizo waweze kuatibiwa mapema kwani kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa saratani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...