
Mwaka wa pili mfululizo, LSF imeshiriki na kuwezesha Kongamano la Kitaifa la Wanawake lenye lengo la kujadili tafiti mbalimbali zilizofanyika katika masuala ya wanawake ili kubaini hali halisi na kuweka mipango mikakati katika kushughulikia masuala ya wanawake katika nyanja ya kiuchumi, kijamii, na kisiaasa kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
"Katika kuendana na ubunifu wa teknolojia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi na kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wote, LSF tumezindua Haki Yangu App inayowezesha kupata elimu ya kisheria, kupata huduma za msaada wa kisheria , kutoa mafunzo maalumu kwa wasaidizi wa kisheria. Kupitia Haki Yangu App, kesi takribani 315 zikiwemo za unyanyasaji wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, migogoro ya ndoa, matunzo kwa watoto zimeripotiwa na kufanyiwa kazi." - Meneja Rasilimali na Mawasiliano LSF, Jane Matinde.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...