Na Kassim Nyaki na Jully Bede Lyimo, Berlin
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe. Dkt Abdallah Possi amezipongeza Taasisi za Serikali zinazoshiriki maonesho ya ITB Berlin na kuzitaka ziongeze juhudi ya kutangaza vivutio vya utalii kidigitali ili kuendana na mfumo wa ulimwengu wa Sayansi na teknolojia.
Mhe. Balozi Possi ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kutembelea banda la Tanzania linalojumuisha Taasisi za Serikali pamoja na makampuni zaidi ya 50 kutoka Sekta binafsi nchini Tamzania yanayoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya ITB Berlin yanayofanyika Jiji la Berlin kuanzia tarehe 7- 9 Machi, 2023.
Mhe Balozi ameeleza kuwa wageni wengi kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa na kasi ya kuhamia katika ulimwengu wa Kidigitali hivyo na sisi watanzania tunapaswa kuendelea kuwekeza nguvu katika teknolojia.
“Ukanda wa nchi za Ulaya mashariki una soko kubwa la watalii wanaoitembelea nchi yetu, tuna Mabango na machapisho mbalimbali katika balozi zetu lakini tunahitaji kuwekeza zaidi kidijitali na kuweka taarifa zote muhimu za masuala ya utalii kwenye mfumo wa QR code ili kuongeza urahisi Kwa wageni wa Mataifa mbalimbali “ ameongeza balozi Possi
Balozi Possi amefafanua kuwa takriban nchi 161 na makampuni ya utalii zaidi ya 5,500 duniani yanashiriki maonesho hayo hivyo ni fursa na soko muhimu kukuza utalii na kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko Tanzania.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...