Na. Damian Kunambi, Njombe.
Katika
kuhakikisha uvuvi wa ziwa nyasa unaimarishwa na kutoa samaki wengi
kulingana na soko, Hatimaye wavuvi wa ziwa hilo wilayani Ludewa mkoani
Njombe wameanza hatua za awali za ufugaji wa samaki kwa kutumia vizimba
baada mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga kuwezesha upatikanaji wa
kizimba kimoja ambacho kimegharimu kiasi cha sh. Ml. 20 kupitia mfuko wa
jimbo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo la kizimba
mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akiwa sambamba na viongozi wa
Chama Cha Mapinduzi wilaya na viongozi wa kata amesema Kizimba hicho
kitakachowekwa samaki ishirini elfu tayari kimewekwa katika eneo la
Chuva lililopo katika kitongoji cha Lutala kata ya Iwela ambako ndiko
mradi huo utakako tekelezwa na kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa sekta
ya uvuvi na kuongeza ajira kwa vijana.
Amesema awali aliwapeleka
kupata mafunzo wataalamu wa sekta ya uvuvi wa wilaya hiyo katika maeneo
mbalimbali ikiwemo mkoani Mwanza na kisha kuleta kufanyiwa utafiti wa
eneo linalofaa kwa uwekezaji huo ambapo eneo hilo la Chuva ndilo lililo
bainika kuwa linafaa kuweka kizimba na kuzalisha samaki hao.
"Ziwa
hili limekuwa likitoa samaki wachache na wadogo huku samaki walio
wakubwa wakibaki ziwani, hivyo katika kipindi hiki niliona ni vyema
kutenga kiasi cha sh. Ml. 20 ili kuweza kuanza na kizimba kimoja na
baada ya hapo tutaendelea kuwekeza zaidi' Amesema Kamonga.
Ameongeza kuwa kwa sasa wilaya hiyo inaelekea katika kuanza kwa miradi
mikubwa kama ya Liganga na Mchuchuma hivyo kufanikiwa kwa mradi huo
kutasaidia kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, pato la halmashauri na
nchi kwa ujimla hivyo vijana wanapaswa kutumia fursa ya mikopo ya
Halmashauri ili kufanya uwekezaji zaidi.
Stanley Kolimba ni
mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilayani humo ambaye pia ni
mwenyeji wa ukanda huo wa mwambao amesema uvuvi uliopo sasa ni uvuvi
usio na manufaa kwani wavuvi wanashindwa kupata samaki wakubwa huku
katibu wa chama hicho ngazi ya Wilaya Gervas Ndaki amesema idadi hiyo
ya samaki watakaofugwa kwa kizimba kimoja ni wengi hivyo vijana watumie
fursa hiyo kwani itawasaidia kuongeza vipato.
Aidha kwa upande wa
wavuvi wa ziwa hilo akiwemo Richard Kayombo wamefurahishwa na kuanza
kwa utekelezaji wa mradi huo huku wakimshukuru mbunge Kamonga, sambamba
na kumuomba kuufanya mradi huo kuwa endelevu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...