Na John Walter-Manyara

Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amezindua mashindano ya Polisi Jamii Cup 2023 yanayofanyika katika wilaya zote tano za mkoa wa Manyara.

Timu 72 za Mpira wa Miguu kwa upande wa wanaume na timu sita za Wanawake netiboli zimejiandikisha kushiriki madhindano hayo yenye lengo la kupinga vitendo vya Ukatili na matukio mengine ya uhalifu mkoani hapa.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaraa Mjini Babati, Twange amewapongeza Polisi kwa kuwa na falsafa ya Polisi Jamii kwani itasaidia kuiweka jamii Karibu na polisi jambo litakalowezesha kupata taarifa za uhalifu kwa urahisi na kuwaondoa Wananchi hofu iliyojengeka kwa polisi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara George Katabazi amesema wameandaa mashindano hayo ikiwa ni utaratibu uliopo chini ya IGP Camillus Wambura lengo likiwa Kutoa elimu juu ya tabia hatarishi na vijana kuwa na afya bora kupitia michezo hiyo kuwaepusha vijana kuacha tabia za matumizi ya dawa za kulevya ,bangi na ulevi ambavyo huchangia kuzorotesha uchumi wa nchi.

Washindi katika michuano hii watapewa zawadi.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...