Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kazi nzuri inayoifanya na kuiasa kuendelea kuwezesha programu ya vijana ya kilimo biashara 'Building a Better Tomorrow' BBT kwa kupatia washiriki wake zana na vitendea kazi vya kilimo kwa muda wa miaka mitatu mfululizo wa programu hiyo.

Rais Samia alitoa pongezi hizo wakati akikagua zana na vitendea kazi vya kilimo vilivyotolewa na TADB Chinangali, Wilaya ya Chamwino kwa ajili ya uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming) iliyo chini ya programu hiyo.

TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na programu hiyo kwa awamu hii ya kwanza.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ( wa tatu kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (wa kwanza kulia) wakati wa uzinduzi wa mashamba makubwa ya pamoja (block farming) uliofanyika jana Chamwino mjini Dodoma. TADB iliwapatia washiriki 812 wa programu ya kilimo biashara Building a Better Tomorrow (BBT) zana na vitendea kazi vya kilimo zenye thamani ya Shilingi milioni mia tano. Kushoto ni Waziri wa Kilimo Hussein Bashe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Frank Nyabundege (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa programu ya kilimo biashara 'Building a Better Tomorrow' BBT muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino mjini Dodoma jana. TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana ambao ni washiriki wa programu ya kilimo biashara 'Building a Better Tomorrow' BBT muda mfupi baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzindua programu hiyo Chamwino mjini Dodoma jana. TADB imetoa zaidi ya shilingi milioni mia tano kununua zana na vitendea kazi vya kilimo kwa ajili ya vijana 812 waliojiunga na program hiyo kwa awamu hii ya kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...