Kwa upande wa Afya amesema kuwa Usafiri huo utaoanzia jijini Dar es Salaam utapunguza jamii kupata matatizo ya afya yanayotokana na uchafunzi wa hali ya hewa pamoja na kupunguza gharama za matibabu ya maradhi mbalimbali hasa yanayosababishwa na uchafuzi wa hali ya hewa.
Kwa Upande wa teknolojia ameeleza kuwa jamii inatakiwa kuwa na uelewa thabiti katika matumizi ya magari ya umeme ambapo kutatakiwa kuwe na muendelezo wa miundombinu pamoja na kuachana teknolojia ya kutumia mafuta ya magari.
"Hii ni mhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania pamoja na kupunguza gharama kwa utumiaji magari ya Umeme."
Magari ya usafiri wa umma yanawajibika na unachangia asilimia 67.4 ya uchagunzi mazingira unaotokana na hewa ukaa.
Akizungumzia kuhusiana na mradi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Makalla amesema kuwa kunafaida kubwa za kujenga miundombinu jijini Dar es Salaam kwa sababu inasaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika na kubeba watu wengi kwa wakati mmoja.
Amesema kuwa sekta ya usafiri inachangia kuleta uharibifu wa mazingira unaotokana na hewa ya Kabonidayoksaidi.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), Dkt. Edwin Mhede amesema kuwa katika Mjadala watajadili namna nchi za Afrika zinaweza kuja na matumizi ya magari yanayotumia nishati rafiki ili kupunguza kiwango cha hewa ya ukaa ambayo huzalishwa kila uchwao kutoka kwenye magari yanayotumia nishati ya mafuta.
Amesema mkutano huo unalenga kujadili kubadili matumizi ya mabasi au magari yanayotumia nishati ya umeme katika majiji yanayoendelea katika nchi za kikanda za Afrika.
Amesema nishati ya umeme inatoa kiwango cha kabonidayoksaidi kwa kiwango cha sifuri kwasababu kunakuwa hakuna makelele wala uchafunzi wa hali ya hewa.
Akizungumzia kuhusiana na Changamoto zilizopo amesema kuwa uelewa wa jamii ni mdogo na Kila jambo linaeleweka kwa kujifunza na kupeana elimu, pia amesema kuanachangamoto za kimuundo ambapo changamoto hizo zinahitaji sera za uhakika, kama sera za kisheria, za kikodi na sera za uwekezaji, sera za fedha.
"Mazingira hayo lazima yafungamanishwe yote ili kutoa motisha ya wawekezaji ambao wanaweza kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji wa magari au watakao agiza magari kutoka nje ya nchi kule nchini kwaajili ya kutoa huduma.
Hata kwa Sisi waendeshaji tunahitaji kupata mazingira wezeshi ya kisera, ambayo yatapelekea kuona thamani ya fedha iliyowekezwa." Amesema Dkt. Mhede
Akizungumzia mradi wa BRT Dkt. Mhede amesema kuwa mtaji mkubwa uliopo Dar es Salaam ni miundombinu kukua kwa kasi na 'icon' Nembo ya BRT Afrika amesema ipo Dar es Salaam pia kwasiku moja wanahudumia watu zaidi ya laki mbili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...