Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw Nurdin Babu amewasihi wafanyabiashara mkoani humo kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotokana na mazingira wezeshi kwao yaliyoandaliwa na serikali pamoja na taasisi za kifedha nchini ambazo zimebuni huduma mahususi zinazoendana na mahitaji yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na benki ya Exim Tanzania mwishoni mwa wiki mahususu kwa wateja hao, RC Babu alisema kwasasa serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kiefedha zimejipanga kuchochea ukuaji wa uchumi kwa kuondoa changamoto mbalimbali zilizoonekana kukwamisha ustawi wa sekta ya biashara nchini hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kuamka na kutumia vema fursa hiyo.

RC Babu alitolea mfano huduma ya Supa woman ya benki ya Exim Tanzania iliyobuniwa mahususi kwa ajili ya wanawake ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kusogeza karibu na kuhamasisha huduma za kibenki kwa jinsia hiyo.

“Wakati serikali ikiwa inaendelea kufanya jitihada mbalimbali zinazolenga kuandaa mazingira bora na wezesha kwa wafanyabiashara, taasisi za kifedha nazo zinaunga mkono jitihada hizi kwa ubunifu zaidi kulingana na mahitaji ya makundi tofauti. Huduma ya Supa Woman na huduma ya Tour Operator account inayotolewa na benki ya Exim ni mfano tosha kwenye hilo. Ni jukumu lenu kuchangamkia fursa hii’’ alisema.

Hata hivyo awasihi wafanyabiashara mkoani humo kutimiza wajibu wao wa msingi wa kulipa kodi pamoja na kuwa waaminifu kwa taasisi hizo za kifedha ikiwa ni ishara ya wao kuonyesha kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali pamoja na taasisi hizo katika kuboresha mazingira bora ya uendeshaji wa shughuli zao.

Awali akizungumza kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ofisa Mkuu Idara ya Fedha Benki ya Exim, Bw Shani Kinswaga aliutaja mkoa wa Kilimanjaro kuwa ni moja ya mikoa ya kimkakati kwa benki hiyo kutokana na ustawi mkubwa wa biashara, kilimo na sekta ya utalii inayofanya vizuri kutokana jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali za kutangaza utalii ikiwemo Mlima wa Kilimajaro.

“Na hiyo ndio sababu Mkoa wa Kilimanjaro umekuwa miongoni mwa mikoa ya awali kabisa kupata fursa ya kusikia mikakati mipya ambayo benki ya Exim tumejiwekea kwa ajili ya wateja wetu ikiwa ni ni hivi karibuni tu tumetoka kuadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwa benki hii. Pamoja na kujipongeza kwa maadhimisho hayo tuliyatumia pia kutafakari na kuamua namna bora zaidi za kuboresha huduma zetu kwa wateja wetu na tupo hapa kuwasilisha na kujadili kuhusu maboresho hayo,’’ alisema.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na bishara za kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo alitumia fursa hiyo kutambulisha huduma mpya za benki hiyo ikiwemo akaunti ya wajasiriamali, akaunti ya Supa Woman, huduma ya benki isiyo na mipaka (borderless banking) mahususi kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro na huduma nyingine za kisasa kwa ajili ya malipo zinazotolewa na benki hiyo kwa ajili ya wafanyabiashara.

“Ujio wa huduma hizi umekuja kuongeza nguvu kwenye huduma kongwe zinazotolewa na benki mahususi kwa wateja wa mkoa huo ikiwemo huduma ya kadi ya Exim TANAPA. Lengo ni kurahisisha huduma zaidi na kuondoa usumbufu kwa wateja wetu na ndio sababu tunawekeza zaidi kwenye huduma za wakala ambapo hadi kufikia sasa tuna mawakala zaidi ya 1000 nchi nzima na tunaendelea kuongeza idadi ya mawakala huku pia tukifanya uwekezaji zaidi kwenye huduma za kielektroniki,’’ alisema Bw Lyimo





Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Bw Nurdin Babu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania mkoani humo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.


Ofisa Mkuu Idara ya Fedha Benki ya Exim, Bw Shani Kinswaga akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoan wa Kilimanjaro iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.


Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na bishara za kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoan wa Kilimanjaro iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.






Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoan wa Kilimanjaro iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.




Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki ya Exim Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa kwenye hafla hiyo.




Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Bw Nurdin Babu (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani humo wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja hao iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...