Benki ya Exim Tanzania imekutana na wateja wake wadogo na wakubwa wa jijini Arusha ili kujadili fursa za biashara, kutambulisha huduma mpya, sambamba na kuwaelimisha wateja hao kuhusu faida na manufaa ya huduma hizo huku Mkuu wa Mkoa huo Bw John Mongella akiipongeza benki hiyo kwa mchango wake katika kuchochea mabadiliko ya kiuchumi ya mkoa kupitia huduma zake kwa wadau mbalimbali wakiwemo wawekezaji kwenye sekta ya utalii, biashara na viwanda.
Akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni
iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki mahususu kwa wateja hao,
RC Mongella alisema mchango wa benki hiyo yenye matawi manne mkoani humo
unaonekana zaidi kupitia huduma zake zinazoendana na mahitaji halisi
ya wateja wake mkoani humo.
“Natoa pongezi hizi nikiwa na
uhakika kwasababu mimi binafsi pia ni mteja wa muda mrefu wa benki ya
Exim na sijawahi kujilaumu kwenye hilo. Katika kipindi cha miaka 20
ambayo mpo hapa Arusha mmekuwa karibu zaidi na wakazi wa mkoa huu mkitoa
suluhisho la huduma za kifedha kulingana na mahitaji na aina uwekezaji
wanaoufanya. Wingi wa matawi yenu mkoani Arusha unathibitisha hilo
hongereni sana,’’ alisema.
Kwa mujibu wa Bw Mongella kwa sasa
mkoa huo upo kwenye kasi kubwa ya mabadiliko ya kiuchumi yanayochagizwa
na ukuaji wa sekta ya utalii, biashara, kilimo na viwanda hivyo
maboresho ya kihuduma yanayofanywa na taasisi za kifedha ikiwemo benki
ya Exim yatakuwa na mchango kwa wadau wengi waliopo kwenye sekta hizo.
“Wito wangu kwenu benki ya Exim na taasisi nyingine za kifedha
muendelee kukutana na wateja wenu mara kwa mara muwasikilize kwa kuwa
mrejesho mtakao upata utawasaidia kubuni huduma zenye majawabu kwao.’’
Alisema RC Mongella huku akionesha kuvutiwa na huduma mpya ya Supa woman
inayotolewa na benki hiyo mahususi kwa wanawake.
Awali
akizungumza kwenye hafla hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw
Jaffari Matundu alisema benki hiyo imedhamiria kufanya maboresho makubwa
katika utoaji huduma kwa wateja wake kwa kutilia mkazo katika maeneo
muhimu, ambayo ni uboreshaji wa mifumo na taratibu za utoaji huduma,
ili ziendane na mahitaji halisi ya wateja na soko.
“Zaidi,
kupitia mkakati huu mpya tumejipanga kuongeza weledi zaidi na umahiri wa
wafanyakazi wetu, kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa pamoja na kukuza
biashara katika nyanja zote ili kuendana na kasi ya Serikali ya awamu
ya sita chini ya uongozi wa Rais Rais Samia Suluhu.’’ Alisema Bw Matundu
aliembatana na maofisa wengine waandamizi kwenye hafla hiyo.
Alisema
imani kubwa inayooneshwa na wateja hao kwa benki hiyo imekuwa sababu
kwao kuwa nao bega kwa bega huku akitolea mfano katika kipindi cha
changamoto za kibiashara zilizowakumba wateja wa benki hiyo hususani
wale waliopo kwenye mnyororo wa biashara ya utalii kutokana na mdororo
wa kibiashara uliotokana na janga la COVID 19.
“Benki ya Exim
tulikuwa pamoja nao na tulichukua hatua za makusudi kwa kuhakikisha
tunatoa likizo ya urejeshaji wa madeni hadi pale hali ya kiuchumi
ilipoanza kurejea katika hali ya kawaida…huu ndio urafiki wa kweli.’’
Alisisitiza.
Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha
wateja binafsi na bishara za kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew
Lyimo alisema utambulisho wa huduma mpya za benki hiyo ikiwemo akaunti
ya wajasiriamali, akaunti ya Supa Woman, huduma ya benki isiyo na mipaka
(borderless banking) mahususi kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Comoro
na huduma nyingine za kisasa kwa ajili ya malipo umekuja kuongeza nguvu
kwenye huduma kongwe zinazotolewa na benki mahususi kwa wateja wa mkoa
huo ikiwemo huduma ya kadi ya Exim TANAPA.
“Lengo ni kurahisisha
huduma zaidi na kuondoa usumbufu kwa wateja wetu na ndio sababu
tunawekeza zaidi kwenye huduma za wakala ambapo hadi kufikia sasa tuna
mawakala zaidi ya 120 nchi nzima na tunaendelea kufanya uwekezaji zaidi
kwenye huduma za kielektroniki,’’ alisema Bw Lyimo huku akisisitiza kuwa
benki hiyo inatoa kipaumbele kwenye huduma za mikopo kwa wateja wa aina
mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa Arusha Bw John Mongella akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa Benki ya Exim Tanzania mkoani humo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoan wa Arusha iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa Arusha Bw John Mongella (Kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bw Jaffari Matundu (kushoto) wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani humo iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Kitengo cha wateja binafsi na bishara za kati wa Benki ya Exim Tanzania, Andrew Lyimo (alievaa koti la bluu) akibadilishana mawazo na baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja hao iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Mkuu wa Matawi wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Agnes Kaganda (kushoto) akiwakaribisha baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoa wa Arusha wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja hao iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wateja wa benki ya Exim Mkoa wa Arusha wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa Arusha Bw John Mongella (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa benki ya Exim Tanzania pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo mkoani humo wakati wa hafla ya chakula maalum kwa ajili ya wateja hao iliyofanyika mwishoni mwa wiki ikilenga kutoa wasaa wa kujadili fursa za kibiashara, mipango ya ukuaji na huduma zitolewazo na benki hiyo katika mkoa huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...