Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza wakuu wa shule zote za sekondari kuwafukuza shuleni wanafunzi wenye matatizo ya nidhamu badala ya kuwasimamisha kwa muda na kusababisha shule za serikali kushindwa kuheshimika.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manyunyu iliyopo Lupembe wilayani Njombe huku akibainisha kuwa hatua hiyo itaongeza wazazi na wanafunzi kuheshimu shule kuliko walimu kutoa adhabu za kawaida kwa wanafunzi na kisha baadaye kuanza kutukanwa na wazazi kwenye mitandao ya kijamii.

"Hatuwezi kufanya shule kama eneo la kuendeshea maungamo,mtoto amekosea nenda kwenye vikao halali na tusilee wala kuvumilia ujinga toa barua ya kufukuza sio kususpend,tukifanya hivyo watu wataheshimu shule za serikali,shule zipo nyingi tena za binafsi zipo hazina wanafunzi fukuza aende kuwatukana wale anaowalipa ada huko"amesema Mtaka

Aidha Mtaka amesema lengo la kufanya hivyo ni kuendelea kulinda walimu kwa kuwa hataki kuona walimu wa mkoa huo wakiendelea kuzalilishwa kwa kutukanwa na yeye yupo tayari kusaini taarifa wakati wowote hata kwa mtandao wa Whatsup kama yupo safarini.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...