Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere ameipongeza RUWASA kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji ikiwa ni azma ya serikali kumtua mama ndoo kichwani.

Ameyaeleza hayo Mjini Babati alipotembelea banda la wanawake katika siku ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani machi 14 badala ya tarehe 8 kutokana uwepo wa ratiba ya ugeni wa katibu Mkuu CCM Taifa.

Amesema uwepo wa miradi hiyo ya maji katika mkoa wa Manyara umesaidia kuwapunguzia wananchi adha ya kutembea mwendo mrefu kufuata maji.

Afisa maendeleo ya jamii RUWASA mkoa wa Manyara Amina Mwanja amesema Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini mkoani hapa wamefanikiwa kumtua mama ndoo kichwani kwa kujenga vituo vya kuchotea maji vya umma 4527 na kufanya maunganisho majumbani kaya 6020 pamoja na kuondoa adha ya muda mrefu ya kufuata huduma ya maji.

Mwanja amesema kuwa katika kutambua uwepo wa wanawake Ruwasa imewapa fursa wanawake kwa kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake.

Amesema RUWASA imeendelea kutoa nafasi mbalimbali kwa wanawake ambapo kuna wajumbe 202 kwenye bodi za maji, wenyeviti 16 wa bodi za maji,mameneja kwenye skimu 12, Wahasibu 30 kwenye skimu, watumishi wanawake kada mbalimbali 37 kwenye ofisi ya RUWASA.

Upatikanaji wa maji maeneo ya vijijini umesaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia kwa pamoja na vitendo vya ubakaji uliokuwa unasababishwa na upatikanaji wa maji kwenye maeneo ya mbali na makazi.

Hata hivyo RUWASA imefanikiwa kupunguza magonjwa kwa wanawake na wasichana kwa kupeleka huduma ya maji mashuleni huku ikiwasaidia wanawake wakati wa kujifungua kwa kupeleka maji kwenye Zahanati na vituo vya afya.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...