Kamanda wa Polisi Mkoa Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya amesema mfanyakazi wa mgodi wa Barrick North Mara, Emmanuel Chacha (26) hakufa kwa kupigwa risasi.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo asubuhi, Kamanda Sarakikya ametupilia mbali taarifa zilizosambazwa kwenye mitando ya kijamii zikidai kwamba mfanyakazi huyo aliuawa kwa kupigwa risasi.

"Maelezo ya watu waliokuwepo kwenye eneo la tukio,na kutokana na matokeo ya uchunguzi wa mwili wa marehemu Emmanuel Chacha uliofanywa na Daktari katika Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kifo chake kimetokana na majeraha yaliyotokana na kujirusha kwenye shimo lenye urefu wa mita 20. Taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kifo cha Emmanuel Chacha kilitokana na kupigwa risasi siyo za kweli, huu ndiyo ukweli", amesema Kamanda Sarakikya.

Kamanda huyo wa Polisi ametoa ufafanuzi huo kutimiza ahadi aliyoitoa Machi 12, 2023 kwamba atatoa taarifa kamili ya kifo hicho baada ya kupata majibu ya uchunguzi wa kidaktari kuhusu mwili wa marehemu huyo.

Katika taarifa yake ya awali, kifo hicho kilichotokea Machi 11, 2023 katika eneo la Gokona Underground ndani ya mgodi wa Barrick North Mara, Kamanda Sarakikya alisema kuwa, kabla ya kujirusha kwenye shimo, timu ya kikosi kazi ilimkukuta mfanyakazi huyo akiiba mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo.

Alieleza kuwa timu hiyo ya kikosi kazi ilijumuisha afisa madini wa mkoa, maafisa kutoka wa jeshi la Polisi, kitengo cha ulinzi cha mgodi huo na kampuni ya ulinzi ya Nguvu Moja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...