Na Janeth Raphael - Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuja na mageuzi makubwa ya elimu kuanzia ngazi za chini mpaka elimu ya juu.

Dkt Franklin Rwezimula ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ameyabainisha hayo leo tarehe 16 machi, 2023 jijini Dodoma katika mkutano ulioandaliwa na Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali, wakuu wa vyuo, Taasisi binafsi, wawakilishi, wanafunzi na watafiti kuzungumzia tadhimini ya awali ya shughuli za Bodi hiyo ya Mikopo nchini.

Dkt Rwezimula amesema mambo watakayojadili ni pamoja na kuona ni kwa namna gani Serikali itasaidia wanafunzi wengi waweze kupata nafasi ya kusoma vyuo vikuu.

"Kama mnavyotambua kwa sasa chanzo kikubwa cha kusaidia wanafunzi wasome ni Bodi ya Mikopo lakini kwa mageuzi tutakayoyafanya wanafunzi watakuwa wengi kiasi kwamba Bodi hawataweza kuwachukua wanafunzi wote." amesema Dkt Rwezimula.

Dkt Rwezimula amesema kuna vyanzo mbalimbali vya kupata fedha ambazo zitasaidia wanafunzi kusoma, hivyo lengo la mkutano huo ni kuangalia mbinu bora ambazo zitasaidia kupata fedha ambazo zitakuwa endelevu kwa ajili ya kusomesha wanafunzi wengi zaidi.

"Serikali inaenda kufanya mageuzi makubwa na tutakuwa na wanafunzi watakaomaliza shule hivyo lazima watoke na ujuzi ambao watapata ajira mitaani"

Aidha Dkt Rwezimula amesema Kongamano hilo litajadili namna bora ya kupata vyanzo hivyo vipya na kuja na maadhimio ambayo yatatoa mwelekeo wa kupata fedha ambazo zitatumika kuhudumia wenye uhitaji.

“Sasa hivi tumepata benki ya NMB, ambao tayari wametenga Sh. bilioni 200 ambapo watu wataweza kukopo kwa ajili ya mikopo ya elimu ya juu na riba yao ni asilimia tisa, kwahiyo bado tunahitaji kupata wadau wengine watakaohudumia watoto wengi katika vyuo vyetu”ameeleza Dkt Rwezimula

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo elimu ya juu Profesa Hamis Dihenga amesema vijana wanazidi kuongezeka tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo hapakuwa na vijana wengi kama sasa kwa mwaka huu 2023 pekee zaidi ya wanafunzi 72 elfu wanaingia na wanahitaji mikopo, hiyo ni idadi kubwa sana.

"Idadi hii imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka sasa kama tukiendelea kutizama tu upande wa Serikali mda mwingine tutakwama sisi tungependa wanafunzi wote wanaostahili wapate mikopo." Profesa Dihenga

Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wq elimu ya juu Zanzibar (ZHELB) Profesa Mohamed Hafidh Khalfan kwa upande wake amesema Uwekezaji katika elimu ni Uwekezaji katika mistakabal wa nchi, wapo watoto wengi wanastahili kuendelea na masomo ya elimu ya juu lakini si kila familia inamudu kulipia watoto wao na kimbilio lao ni Bodi ya Mikopo.

" Katika mkutano huu tutatafakari haya yanayotukabili, tunakotoka tulipo na vipi tunajiandaa kwa tunakokwenda ili hatimaye vijana wetu wenye uwezo wapate nafasi ya kuendelea na masomo" - Profesa Khalifa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB) Abdul-Razaq Badru amesema wanazungumzia tathimini ambazo ni kutazama kama Serikali, Bodi ya Mikopo wale wanaolipiwa pesa na program wanazosoma ni za aina gani na kwa kiasi gani digirii wanazosoma zinawiana na mahitaji ya soko la ajira

"Hii itaisaidia Serikali kufahamu kwamba Uwekezaji wake unaelekea katika maeneo ambayo ni muafaka na yanayoshabihiana na mahitaji ya soko" - Badru.

Naibu Katibu mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula,akiwa katika picha na washiriki mara baada ya kufungua  kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.

Naibu  Katibu mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk.Franklin Rwezimula,akizungumza wakati  akifungua kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.

Mkurugenzi  Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Abdul- Razaq Badru ,akizungumza wakati  wa kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya mikopo wanafunzi wa elimu ya juu Zanzibar (ZHELB) Prof.Mohammed Hafidh Khalifa,akizungumza wakati  wa kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB)Prof. Hamis Dihenga ,akizungumza wakati  wa kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.

Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali  wakati  wa kongamano la kujadili namna  ya kupata vyanzo vipya vya mapato vitakavyo tumika kuhudumia wanafunzi wa elimu ya juu nchini (HESLB) lililofanyika leo Machi 16,2023 jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...