Na Mwandishi Wetu
TAASISI
ya Wanawake na Diplomasia, imetoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea
kutumia diplomasia kuifungua nchini katika nyanja mbalimbali ikiwemo ya
uchumi na diplomasia.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam
kwenye Kongamano maalum lililoandaliwa na Taasisi ya Wanawake na
Diplomasia na kuhusisha mabalozi, wanadiplomasia kutoka taasisi na
kampuni mbalimbali, Mwanadiplomasia mkongwe Balozi Liberata Mulamula
ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo Rais Samia amekuwa kinara wa
diplomasia.
“Diplomasia inatumika katika mambo mengi yakiwemo
kuangalia jinsi gani mnaweza kutatua mifarakano, matatizo kwa njia za
mazungumzo, kwa njia zuri na huenda wanawake tumezaliwa na huo ujuzi ,
nimefarikijika kwani mwaka jana taasisi hii ilipotukutanisha kulikuwa na
wanawake kutoka Serikalini.
“Wanawake wanaojulikana sana lakini
leo tumekuwa na wanawake ambao wametoka kwenye eneo la biashara na
tunafahamu hata katika kufanya bashara unatumia diplomasia katika
kuvutia biashara yako.Hivyo wakati leo tuaadhimishi siku ya wanawake
duniani hawa vijana wameamua tuwe na siku maalumu.
“Kwani huwa
tumekuwa tunazungumzia, wanawake katika siasa, wanawake katika biashara
lakini leo hii ni wanawake katika diplomasia mimi mnajua ni kama
nilizaliwa kwenye diplomasia, nimezeeka kwenye diplomasia lakini hawa
vijana wamechukua jukumu la kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuzalisha
wana diplomasia,”amesema Balozi Mulamula.
Aidha amesema Tanzania
kwenye eneo la diplomasia iko vizuri na ndio maana haina nchi adui ,
hiyo inatokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mwalimu Julius Nyerere na
sasa chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan diplomasia imepaishwa zaidi,
amefungua nchi, dunia yote inaangalia Tanzania.
“Ujumbe wangu kwa
vijana kwanza mjiamini na mjue inawezekana, jenga mahusiano , ipende
kazi unayofanya na muhimu jiheshimu , jiongoze. Kuhusu miaka miwili ya
Rais Samia hasa katika nyanja ya Diplomasia kuna mengi ya kusherehekea
pengine inahitaji kupindi maalumu.
“Rais amefungua nchi ambayo
imetuletea neema , imetuletea faraja katika maeneo yote, diplomasia
imepaa , amepanga safu nzuri ya diplomasia kutoka nyanja mbalimbali
maana zamani ilikuwa mwana diplomasia lazima atoke Wizara ya Mambo ya
Nje lakini yeye amechanganya uzoefu mbalimbali na Tanzania inafika.
“Tunamshukuru
sana Rais wetu na leo kwenye jumuiko nilikuwa nawaambia mtu usijifanye
sijui nani , kuwa wewe, mnavyomoona Mama Samia ni Mama Samia,
tunampenda, tumheshimu, kwa hiyo katika miaka miwili yako mengi na mimi
nilipata bahati ya kuhudumu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje kwa zaidi
ya mwaka mmoja na nusu na tarehe 19 anapotimiza miama miwili ya uongozi
wake tutakutana pamoja kwa ajili ya kumpongeza.
Kwa upande wake
Balozi wa heshima wa Seychell Maryvyonne Poll ambaye amekuwepo nchini
Tanzania kwa mwaka wa 41 sasa amesema Rais Samia amekuwa mstari wa mbele
kwenye eneo la diplomasia na tangu ameanza kazi ametumia diplomasia
katika kutekeleza masuala mbalimbali.
“Diplomasia sio tu lazima
kuwa balozi bali wanawake wote ni mabalozi kuanzia nyumbani, katika
biashara na ukweli kwa sasa wanawake tunamfuata Mama samia kwasababu
yeye ni Mwanadiplomasia namba moja kwa hapa nchini Tanzania,”amesema
Balozi Pool.
Kuhusu kongamano lililoandaliwa na Taasisi ya
Wanawake na Diplomasia amesema amefurahi kwani amekutana na wasichana
wengi na vijana wa Shule ya diplomasia Kurasini, ujumbe wake amewaomba
kutokana tamaa ili kufanikisha ndoto yao ya kuwa wana diplomasia na wala
wasiogope.
Wakati huo huo Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi
ya Wanawake na Diplomasia Kaneni Mushi amesema tukio hilo
limewakutanisha mabalozi, wanawake wa taasisi mbalimbali pamoja na
vijana wanaosomea diplomasia.Lengo kuu ni kumsherehekea mwanamke katika
sekta nzima ya diplomasia lakini kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia
Suluhu Hassan ambaye ndiyo mwanadiplomasia namba moja nchini kwa namna
anavyopeperusha bendera anavyofungua uchumi na kulifanya taifa kujulina
duniani.
Ametumia nafasi hiyo kueleza taasisi hiyo imejikita
katika uchumi wa diplomasia , hivyo wanashukuru wadau wengi kujitokeza
huku akieleza kufunguliwa kwa milango ya diplomasia nchini wanashuhudia
maendeleo yanavyoongezeka.
“Tanzania tunatambulika,tunaheshimika
, tunaona vijana wengi wanafanya vitu vikubwa, wana kampuni zao, wana
taasisi zao, hivyo tunamshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa jinsi
ambavyo amefungua diplomasia ya uchumi.”
Matukio
mbalimbali katika picha wakati wa Kongamano la Diplomasia
lililoandaliwa na Taasisi ya Wanawake na Diplomasia kwa ya kujadiliana
masuala ya diplomasia ikiwemo ya uchumi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...