Na Muhidin Amri,Madaba

WAKALA wa barabara za vijijini na mijini(Tarura)imekamilisha ujenzi wa daraja lililojengwa kwa teknolojia ya mawe katika mto Mgombezi linalounganisha kijiji cha Lipupuma,Mgombezi na Chechengu katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.

Meneja wa Tarura wilaya ya Songea Bakari John alisema,daraja la mto Mgombezi lina urefu wa kilomita 41 na ujenzi kwa kutumia teknolojia ya mawe ni wa gharama nafuu na la kwanza kujengwa wilayani Songea.

Alitaja gharama za ujenzi wa daraja hilo ni shilingi milioni 152 tu na kueleza kuwa, kama wangejenga kwa kutumia zege na chuma kama ilivyo kwa madaraja mengine basi serikali ingetumia zaidi ya shilingi milioni 500.

Alisema,kabla ya ujenzi wa daraja hilo wananchi walilazimika kupita kwenye daraja la miti lililojengwa na wananchi wenyewe,hata hivyo wakati wa masika halikuwasaidia kutokana na mto Mgombezi kujaa maji mengi na kukatisha mawasiliano kati ya upande mmoja na mwingine.

Alieleza kuwa, kujengwa kwa daraja hilo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo kwani limetatua kero ya muda mrefu ya usafiri na usafirishaji wa mazao hasa mbao na Tangawizi.

Meneja huyo wa Tarura aliongeza kuwa, kazi iliyobaki ni kuendelea kufungua barabara za kuunganisha mashamba ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zao za kilimo kwa urahisi.

Baadhi ya wananchi waliokutwa wakivuka katika daraja hilo,wameishukuru serikali kwa uamuzi wake wa kujenga daraja la kudumu kwani kwa muda mrefu walikuwa wakiteseka kupita kwenye maji pindi wanapohitaji kuvuka upande mmoja kwenda mwingine.

Nuru Francis mkazi wa Lipupuma alisema,walikuwa na hali mbaya kwani walilazimika kupita kwenye mto huo wenye maji mengi kila siku na wakati wa masika walishindwa kwenda kwenye shughuli zao za uzalishaji mali kutokana na mto huo kujaa maji.

Michael Brumo,ameipongeza serikali ya awamu ya sita kuona umuhimu wa kujenga daraja katika eneo hilo kwa sababu ilikuwa changamoto kubwa kila wanapotakakusafirisha mazao yao kutoka shambani kwenda sokoni.

Robert Mbilinyi,ameishauri serikali kuendelea kujenga madaraja kwa kutumia teknolojia ya mawe ambayo ni ya gharama nafuu na kuachana na ujenzi wa madaraja ya chuma ambayo wakati mwingine baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu wanahujumu kwa kuiba vyuma na hivyo kuisababishia serikai hasara kubwa.


Daraja la mto Mgombezi lililojengwa kwa teknolojia ya mawe na Wakala wa Barabara za vijijini na mijini Tarura wilaya ya Songea ambalo limesaidia kuunganisha vijiji mbalimbali vya kata ya Mkongotema Halmashauri ya wilaya Madaba.

Magari na pikipiki yakianza kupitika katika daraja la mto Mgombezi Halmashauri ya wilaya Madaba lililojengwa kwa kutumia mawe badala ya chuma linalounganisha vijiji mbalimbali katika kata ya Mkongotema Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma.

Muonekano wa sehemu ya juu ya daraja la mto Mgombezi lililojengwa kwa teknlojia ya mawe na wakala wa Barabara za vijijini na mijini TARURA wilayani Songea kwa gharama ya shilingi milioni 152 ambalo ni kwanza kujengwa kwa kutumia mawe wilayani Songea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...