NA FARIDA MANGUBE. MOROGORO.
Shirika la Reli Tanzania (TRC) imeanza kujenga ushoroba wa mnyama tembo ili kudhibiti muingiliano baina ya mnyama huyo na njia ya reli ya kisasa katika eneo la Ngerengere kipande cha Morogoro- Dar-es-salaam baada ya kuongezeka kwa matakwa ya kimazingira.
Akitoa taarifa ya ujenzi huo mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge ya hesabu za serikali (PAC) ,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Masanja Kadogosa amesema kutokana na Tembo kuwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbuku za Mapito yake kwa zaidi ya miaka kumi hivyo wameona ni vyema kuweka ushoroba utakaodaidia kupunguza Ajali.
Amesema kipande cha Morogoro - Dar es salaam kimefikia asilimia 97.7 na kwamba kukamilika kwa reli hiyo kutawezesha kukuwa kwa sekta ya madini nchini hususani makaa ya mawe yatakayosafirishwa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine ikiwemo nje ya nchi.
Kwa upande Makam Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Japhet Hasunga ameipongeza Serikali kupitia Shirika la reli Tanzania kwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya awamu tana na Sita
"Kamati yangu kushuhudia mabehewa manzuri mabehewa mapya kabisa ni tofauti na yale tuliyokuwa tukiyaona kwenye mitandao ya kijamii kwamba ni mabehewa ya zamani, mabehewa tuliyoyaona leo ni mapya kabisa na nimanzuri japo yanarangi ya TRC ya zamani"alisema Asunga
Aidha amewata watanzania hasa wakulima kuongeza uzarishaji ili kutumia fursa iliyopo kwenye uwekezaji wa reli ya kisasa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...