WASICHANA wametakiwa kutumia mafunzo wanayoyapata ya ujasiriamali kwa ajili ya kujiinua kiuchumi na kuchangamkia fursa watakazoziona na kutokatishwa tamaa na maneno ya watu na kushindwa kushiriki katika masuala ya kimaendeleo.
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Brac Maendeleo Tanzania imeendelea kushiriki katika maendeleo ya kumuinua mtoto wa Kike na kuunga mkono juhudu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuwezesha mtoto wa kike kujiinua kiuchumi kwa kumpatia elimu na mafunzo ya ujasiriamali.
Meneja Mkuu wa Fedha na Rasilimali Brac, Shukuru Musabila amesema wamekuwa na miradi mingi ya kuwawezesha mabinti wa kike kuweza kupata ujuzi sambamba na kuwapatia elimu ya ujasiriamali wakishirikiana na wazazi wa watoto hao na pindi wanapomaliza wanapatiwa vifaa kwa ajili ya kuanza kujiinua kiuchumi.
Shukuru amesema, Brac imekuwa na miradi mingi tofauti ya kusaidia wakina mama na wasichana inayojulikana kama Goal ambapo kwa sasa inaendelea katika maeneo ya Buguruni na Vingunguti na hapa wamekuja kwa ajili ya kuwakabidhi vifaa wasichana 270 waliohitimu mafunzo yao ya miezi mitatu katika fani mbalimbali.
Amesema, watakabidhi vifaa hivyo kwa wahitimu wa ushonaji, vifaa vya urembo, mapishi na thamani ya vitu vyote ni takribani milioni 100.
Mbali na mradi wa Goal kuna mradi wa AIM ambapo rasmi ilianza rasmi mwaka 2019 na inapatikana pia katika mikoa mitano tofauti nchini ambayo ni Pwani, Dodoma, Singida, Morogoro na Dar es Salaam
"Lengo la Brac ni Kumuwezesha mtoto wa kike aweze kujisimamia mwenyewe na miradi hiyo ni kwa ajili ya kuwapatia ujuzi na kuwawezesha kiuchumi kwa kuwapatia vifaa baada ya kumaliza mafunzo yao.
Amesema ,"kwa sasa Wasichana 270 wamehitimu mafunzo hayo kupitia Veta na Club meongeza kuwa takribani wasichana zaidi ya 600 walipata mafunzo hayo na kuhitimu na wengine kuwezeshwa kiuchumi kwa kuwapatia vifaa vya kufanyia kaz
Aidha, Brac Tanzania imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo kwa kushiriki katika miradi ya uwezeshaji wakina mama nchini na kuwahamasisha wanawake kujiunga na Vikundi kwani vimekuwa vinawasaidia katika kujiinua kiuchumi na kwa Mkoa wa Dar es Salaam wamekuwa na Club 15 kwenye maeneo ya Ilala na Vingunguti.
Meneja Mkuu wa Fedha na Rasilimali Kutoka Brac Maendeleo Tanzania (katikati) akikabidhi Vifaa kwa wahitimu wa mafunzo ya ujasiriali na elimu ya afya kupitia mradi wa Goal unaoendeshwa na taasisi ya Brac Maendeleo Tanzania. Wasichana 270 wamehitimu mafunzo hayo katika fani mbalimbali ikiwemo Urembo, Upikaji wa Keki, Ushonaji na zinginezo. Kushoto Ni Meneja Mradi wa Vijana na Uwezeshaji Kutoka Brac Upendo Daudi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...