Katika kuadhimisha Siku ya Maji Duniani, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imesisitiza dhamira yake katika mipango ya utoaji wa maji safi na salama kwenye jamii za watanzania pamoja na kulinda vyanzo vya maji, huku wafanyakazi wake wakiungana na watanzania kufanya usafi mto Mirongo jijini unaopeleka maji yake Ziwa Victoria jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo lililofanyika jana, Meneja wa Mawasiliano na Mambo Endelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema kampuni hiyo iko tayari kuendelea kuwekeza kwenye juhudi za kulinda vyanzo vya maji sawa sawa na kauli mbiu ya mwaka huu. Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya maji duniani ni kuongeza mabadiliko kupata suluhisho la mgogoro wa maji safi.

Mto Mirongo unaopita jijini Mwanza ni mchafu sana na mara nyingine wakazi wa eneo hilo hulaumiwa kwa kutupa uchafu kwenye mto huo hasa hasa wakati wa mvua, kitu ambacho kinaweza kuathiri afya zao na kusababisha magonjwa kama kipindupindu. Zoezi la usafi wa mto huo lilifanya na wafanyakazi wa SBL kwa kushirikiana na Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria.

Hatibu alisema SBL imefanikisha mambo mengi yanayohusiana na huduma za maji na utunzaji wake ikiwemo miradi mikubwa 24 ya maji nchini ndani ya miaka kumi iliyopita ambapo miradi hiyo kwa pamoja imenufaisha watu milioni 2 na maji safi na bure kupitia programu yake ijulikanayo kama ‘Water of Life’.

“SBL itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuwezesha jamii zenye uhitaji wa maji safi na salama kupata maji. Hii ni ahadi tuliyojiwekea chini ya mpango kazi wetu tunaouita ‘Society 2030,” alisema.

Mapema mwezi huu, SBL iliwekeza jumla ya Tsh milioni 380 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa bwawa la maji la Kwamizi wilayani Handeni, mkoani Tanga. Baada ya kukamilika mradi huo unatarajiwa kunufaisha maelfu ya wakazi katika wilaya hiyo.









Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) tawi la Mwanza wakifanya usafi mto Mirongo uliopo jijini Mwanza kama sehemu ya kuadhimisha siku ya Maji Duniani. Mto Mirongo hupeleka maji Ziwa Victoria. Kwenye zoezi hilo, wafanyakazi wa SBL walishirikiana na Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...