Na Mwandishi wetu Dodoma.

Wakala wa usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) wamefanikiwa kuongeza idadi ya maeneo ya kazi yaliyosajiliwa kutoka 4,336 hadi 11,953 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 276.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji Mkuu OSHA Khadija Mwenda leo jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya wakala wa usalama na afya mahala pa kazi ( OSHA)

Mtendaji Khadija amesema idadi ya kaguzi zilizofanyika zimeongezeka kutoka kaguzi 104, 203 hadi kufikia kaguzi 322, 241 sawa na asilimia 132, na kumekuwa na ongezeko la asilimia 175 ya wafanyakazi waliopata mafunzo ya usalama na afya mahala pa kazi kutoka 32, 670 hadi kufikia wafanyakazi 43, 318.

Mafunzo hayo yanajumuisha mafunzo ya usimamizi wa masuala ya usalama na afya mahali pa kazi na uundwaji wa kamati za Usalama na Afya (Health and Safety Managemnet System), mafunzo ya kufanya kazi za mazingira ya juu (working at height), mafunzo ya huduma ya kwanza, mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali katika maeneo ya kazi, mafunzo ya usalama na afya katika sekta ya mafuta na gesi na katika sekta ya ujenzi na majenzi, mafunzo ya usalama wa mitambo.

Aidha, kumekuwa na ongezeko la upimaji afya za wafanyakazi kwa asilimia 320, Upimaji afya kutoka Wafanyakazi 363,820 hadi kufikia Wafanyakazi 1,112,237 waliopimwa katika kipindi tajwa.

"Ongozeko hilo lilitokana na kupunguza ada mbalimbali na kuboresha mifumo ya usimamizi ambayo imewezesha maeneo mengi ya kazi kukaguliwa, wafanyakazi wengi kupimwa afya na mafunzo mbalimbali kufanyika, ongezeko hili ni tafsiri kwamba hali ya usalama na afya katika maeneo ya kazi inazidi kuimarika." amesema Mkurugenzi Khadija.

Hata hivyo Khadija amesema katika kusimamia Sheria ya Usalama na Afya kwa lengo la kuzuia ajali, magonjwa na vifo vitokanavyo na kazi, maeneo ya kazi ambayo hayakuzingatia Sheria na Kanuni za Usalama na Afya yalichukuliwa hatua mbali mbali za kisheria zikiwemo kupewa hati ya maboresho (Improvement Notice) ambapo maeneo ya kazi 1,588 yalipewa hati hizo na maeneo ya kazi mengine 105 yalitozwa faini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA)  Khadija  Mwenda akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati akieleza utekelezaji wa majukumu ya OSHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...