.jpg)
Meneja
Matengenezo kituo cha kutunza taarifa cha kampuni ya Vodacom Tanzania
mkoani Dodoma, Mhandisi Josiah Kizinda akitoa ufafanuzi namna mitambo
inavyofanya kazi kwa wanafunzi wa kike 96 kutoka baadhi ya shule za
sekondari zilizoko katika mikoa ya Kanda ya Kati. . Ziara hiyo
iliandaliwa na mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kuwahamasisha
wasichana kupenda masomo ya Sayansi na TEHAMA chini ya mpango wa ‘Girls
in ICT’ unaoratibiwa na serikali kupitia mfuko huo.
Meneja
Matengenezo wa kituo cha kutunza taarifa za kampuni ya Vodacom Tanzania
Plc jijini Mbeya, Mhandisi Adamu Mndeme akitoa ufafanuzi namna mitambo
inavyofanya kazi kwa wanafunzi wa kike 56 kutoka baadhi ya shule za
sekondari zilizoko katika mikoa saba ya Nyanda za Juu Kusini. Ziara hiyo
iliandaliwa na mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kuwahamasisha
watoto wa kike kupenda masomo ya Sayansi na TEHAMA chini ya mpango wa
‘Girls in ICT’ unaoratibiwa na serikali kupitia mfuko huo.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...