Na Mwandishi Wetu,Iramba
WANANCHI wilayani Iramba mkoani Singida wamempongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kutoa ruzuku ya mbolea kwa wakulima kwa ajili ya msimu huu wa kilimo na kwamba wameanza kuona matokeo ya ruzuku waliyopewa na Rais.
Wakizungumza leo Machi 1,2023 mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ambaye yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi , wananchi wa Kata ya Ulemo wilayani Iramba mkoani Singida wamueleza Katibu Mkuu huyo kwamba wameanza kuona matokeo ya mbolea ya ruzuku kwenye mashamba yao, hivyo wanatoa shukrani kwa Rais Samia.
Mkulima na Mkazi wa Kata ya Ulemo Peter Paulo amesema kwamba kwa muda mrefu mrefu wamekuwa wakipata changamoto kwenye bei ya mbolea lakini Rais Samia baada ya kutoa ruzuku kwenye mbolea mwaka huu kwenye msimu wa kilimo wameanza kuona matokeo yake kwenye mashamba yao.
Kwa kukumbusha tu bei ya mbolea katika soko la Dunia imepanda katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kutokana na janga la corona,vita ya Urusi na Ukraine na athari za uchumi duniani hali iliyofanya mfuko mmoja wa mbolea kufika shilingi 145,000 kutoka shilingi 60,000.
Hata hivyo Rais Samia Agosti mwaka 2022 akiwa kwenye kilele cha Maadhimisho ya sikukuu ya wakulima mkoani Mbeya alizindua mpango wa utoaji ruzuku kwa wakulima na kusema katika msimu wa mwaka 2022/23 serikali imetoa shilingi bilioni 150 kusaidia bei ya mbolea kushuka.

.jpeg)

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Mwenyekiti wa shina namba 6 Ndugu Evangelina Petro Samuel,wakati wa kikao cha wanachama wa CCM wa shina hilo katika Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Iramba,mkoani Singida

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Iramba Ndugu Mwigulu Mchemba (kushoto) wakati wa kikao cha wanachama wa CCM wa shina namba 6, Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Uramba, katikati ni Mwenyekiti wa shina hilo Ndugu Evangelina Petro Samuel.

.jpeg)
wanachama wa CCM wa shina namba 6, Tawi la Ulemo Kata ya Ulemo wilayani Uramba wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo

Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Ndugu Issa Ussi Gavu

Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa itikadi na Uenezi Sophia Mjema akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango Mhe Mwigulu Nchemba wakati wa mkutano maalum wa Balozi wa Shina namba sita,katika kata ya Ulemo wilayani Iramba,mkoani Singida.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...