Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inatarajia kutangaza kampuni bunifu chipukizi tatu zilizoibuka washindi wa msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator iliyofanyika kwa kushirikiana na Smart Lab.
Washindi watapatikana baada ya kuwasilisha na kuonyesha shughuli wanazozifanya kwa jopo la majaji waliobobea kwenye maeneo ya teknolojia, ujasiriamali, uwekezaji, na sheria. Uwasishaji wa maonyesho hayo unatarajiwa kufanyika siku ya Machi 3, katika hoteli ya Hyatt Regency ya jijini Dar es Salaam.
Ikiwa imebuniwa kwa ajili ya kampuni bunifu chipukizi zinazoamza kujiendesha kwa faida, msimu wa pili wa programu ya Vodacom Digital Accelerator ulianza mwezi Aprili mwaka 2022 na kuruhusu maombi kutoka kwa kampuni zote bunifu chipukizi za kiteknolojia za Kitanzania zenye mustakabali wa kukua.

Kutoka mamia ya maombi yaliyopokelewa, kampuni 12 zilichaguliwa kujiunga na programu hii na kuingia kwenye hatua ya kujengewa uwezo ambapo zilipatiwa msaada wa ziada kwenye kukuza mikakati yao ya kimasoko, eneo la kiufundi, na kuwaunganisha kwa washirika na wawekezaji.
Kampuni hizo bunifu chipukizi zinatoka kwenye sekta tofauti ambazo ni Pamoja na huduma za kiteknolojia za kifedha, afya, biashara za mtandaoni, elimu, kilimo, na usalama wa mtandaoni.
“Tumefurahi kufikia hatua hii ya programu yetu ya Vodacom Digital Accelerator ambapo tumefanikiwa kuona namna ilivyosaidia kukuza ubunifu kwa kampuni chipukizi za Kitanzania, uwasilishaji tutakaojionea kwenye maonyesho ndio utasaidia kuwatambua washindi watatu, ambao watazawadiwa Zaidi ya Shilingi milioni 200 za Kitanzania za msaada wa kulingana na thamani Pamoja na uwezekano wa uwekezaji zaidi mbeleni. Ningependa kutoa wito kwa wadau kwenye sekta ya ubunifu na teknolojia kujisajili kwa njia ya mtandaoni ili kushiriki wakiwa popote walipo siku ya kesho,” alisema Bw. Nguvu Kamando, Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali, Vodacom Tanzania PLC.
Watu wote wanakaribishwa kujiunga nazi, au kusikiliza uwasilishaji wa maonyesho hayo na kuweza kuzipigia kura kampuni bunifu chipukizi bora kupitia kiambatanisho (link) ambacho kitapatikana kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya kampuni.
Kampuni bunifu chipukizi ambazo zimefikia hatua ya fainali ni pamoja na Shule Yetu Innovations, Smart Darasa, Lango Academy, na Vijana Tech, kwa upande wa huduma za elimu za kiteknolojia. Hack it Consultancy inawakilisha eneo la huduma za usalama wa mtandaoni. Seto, Twenzao, Get Value, na Spidi Africa zipo chini ya biashara za mtandaoni. Nyinginezo ni Medpack ikiwakilisha huduma za afya za kiteknolojia, zikiwemo na, Bizy Tech Pamoja na Bizzy Pay ambazo zenyewe zipo upande wa huduma za kifedha za kiteknolojia.

Mkurugenzi wa Huduma za Kidigitali wa kampuni ya teknolojia ya
mawasiliano Vodacom Tanzania Plc, Nguvu Kamando (katikati ya waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa programu ya Vodacom Digital
Accelerator inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Plc kwa kushirikiana na
Smart Lab.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...