Na Janeth Raphael - Michuzitv Dodoma

Imeelezwa kuwa wananchi wengi hawapo tayari kujitolea kuwachangia  ndugu na jamaa zao walio na maradhi ya figo wenye vigezo  na uhitaji wa kupandikiza, kwa kujengewa hofu au kuhofia matokeo ya uchangiaji yanaweza kuleta adhari za kiafya.

Mkurugenzi Mtendaji  wa Hospitali ya Kanda  ya Benjamin Mkapa iliyopo jijini Dodoma Dkt Aliphonce Chandika ameyaeleza hayo leo February 13, 2023 ikiwa ni maadhimisho ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika hospitali hiyo.

Katika maandalizi ya kuanza huduma hiyo ya kupandikiza figo wataalamu wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na chuo kikuu cha Dodoma walianza kwenda mafunzoni nchini Japan mwaka 2017, mpango huo wa kuwajengea uwezo wataalamu hao ulikuwa wa miaka mitano kuanzia mwaka 2012-2022 kwa kushirikiana na Tokushukai Medical Group kutoka Japan.

Dkt Chandika amesema mtu anayechangia figo yupo salama na hatopata  madhara yoyote ya kiafya kwa sababu ya kuchangia figo.

" Nasema haya kwa uhakika kabisa tuna watu 33 waliochangia figo kwa kunusuru maisha ya ndugu au jamaa zao hapa hospitali  ya Benjamini Mkapa Dodoma na hakuna hata mmoja kati yao amewahi kurudi akiwa na shida iliyotokana na kuchangia figo,  jambo hili ni salama tujitoe kuokoa ndugu zetu" - amesema Dkt Chandika.

Mpaka sasa hospitali hiyo imefanikiwa kupandikiza  wagonjwa  thelathini na tatu (33) na kati ya hao wagonjwa ishirini na mbili (22)  walipandikiza figo  na wataalamu wazawa 

" Ni furaha yangu kuwa kwa sasa wataalamu wetu wanafanya zoezi hili wao wenyewe bila ya kuwepo kwa usimamizi wa wataalamu hao kutoka Japan haya ni mafanikio makubwa" - Dkt Chandika

Gharama za matibabu kumpeleka mgonjwa kutibiwa nchini India ni fedha za Kitanzania milioni 77 mpaka 80. Lakini  kwa mgonjwa kufanyiwa upandikizaji wa figo hapa nchini kupitia Hospitali ya Benjamin Mkapa inagharimu fedha za Kitanzania milioni thelathini na tano (35)tu.

"Huu ni ugojwa ambao mtu unatakiwa uwe na fedha za kutosha kuanzia usafishaji wa damu ( Dialysis ) ambao ni hatua ya mwanzo kabla ya kufanya upandikizaji wa figo, mgonjwa hutakiwa kusafisha damu walau mara tatu kwa wiki ambayo humgharimu fedha za Kitanzania shilingi laki saba na nusu (750,000) mpaka laki tisa 900,000).

Naye Daktari Bingwa wa magonjwa ya  figo Alfred Miremo amesema kumekuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa ya figo kwa sababu ya mtindo wa maisha tunayoishi, hapo zamani kulikuwa na vitu vingi vya kufanya kama mazoezi, kula nyumbani vyakula vya asili, lakini kwa sasa kuna ulaji usio salama kama chips mayai, kwa kiasi kikubwa tumejiingiza katika mabadiliko ya maisha na mwisho  miili inaongezeka na kuwa wanene kupita kiasi

"Magonjwa kama shinikizo la juu yanaanza kuingia ki msingi Tanzania nzima shinikizo la damu ya juu linaongoza kwa kusababisha madhara kweye figo zetu. Na ugonjwa wa kisukari unachangia pia kwa wale wenye tatizo hilo endapo hawafati masharti, matumizi holela ya dawa ikiwepo mitishamba na dawa za maumivu ambazo hazijadhibktishwa na daktari' - amesema Dkt Miremo.

Hata hivo Dkt Miremo amesema kuwa ki msingi mwanadamu ana figo mbili na  ana uwezo wa  kuishi na figo moja bila changamoto yoyote ile kwa kuwa kabla mtu hajatolewa figo hiyo wataalamu huwa wanafanya uchunguzi na kujiridhisha kabla ya kutoa figo hiyo hivyo amewaasa wananchi kuwasaidia ndugu au jamaa wenye uhitaji wa figo ili kunusuru maisha yao

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma Dkt Aliphonce Chandika akizungumza leo  katika kilele cha maadhimisho ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika hospitali hiyo.
Daktari bingwa wa magonjwa ya Figo Alfred Miremo akizungumza katika maadhimisho ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa  jijini Dodoma.
Baadhi ya wataalamu kutoka Tokushukai Medical Group nchini China wakifuatilia jambo katika maadhimisho ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.

Baadhi ya madaktari wa Hospitali ya Kanda ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma wakifuatilia jambo katika maadhimisho ya miaka mitano ya upandikizaji figo katika hospitali hiyo yaliyofanyika leo jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...