Na Rosena Suka Lushoto
KATIKA kuhakikisha mtoto wa kike anawezeshwa kuhudhuria masomo na kupata elimu pasi na kufikiria changamoto ya kukosa taulo za kike awapo masomoni, na kumpunguzia changamoto hii kama si kuimaliza kabisa, leo Machi 7, 2023 kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, wanawake wanaofanya kazi katika Taasisi za umma na binafasi Wilayani Lushoto wamekabidhi jumla ya maboksi 15 ya taulo za kike kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bi. Ikupa Mwasyoge.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, Bw. Eliza Moses wakati wa kupokea msaada huo uliotoka kwa wanawake kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, na Taasisi binafsi ya Usambara Development Instiative aliwashukuru sana kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia watoto wa kike walioko katika shule za msingi na sekondari wilayani humo. Bw. Elieza aliendelea kwa kuziomba taasisi nyingine zijitokeze kusaidia wanafunzi na kuelekeza kwamba ugawaji wa taulo kwa watoto wa kike iwe ni kampeni maalumu ya kunusuru na kuwakomboa watoto wa kike.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye ni Mratibu wa Maadhimisho ya siku wa wanawake Duniani Bi. Fortunata Metusela akiongea kwa niaba ya Mkuurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na wakati wa ugawaji wa Taulo hizo kwa wanafunzi hao aliwaeleza kwamba wamepata msaada huo kwa ajili ya kuwastiri wakiwa katika siku za hedhi wanafunzi hao wasikose vipindi vya masomo wanapokuwa katika siku zao.

Bi. Metusela aliwasisitiza wanafunzi hao kuwa upatikanaji wa taulo za kike kwao ni msaada mkubwa ili kufanya vizuri kitaaluma kwa sababu hawatakosa vipindi vya masomo bali watahudhuria vyote, na kutoa wito kwa wanafunzi wafanye vizuri kitaaluma na kupata ufaulu mzuri. Aidha aliwawataka wanafunzi wa kike kujiepusha na mazingira hatarishi ya kufanyiwa ukatili wa kijinsia na endapo watakufanyiwa vitendo hivyo watoe taarifa kwa viongozi, wazazi au walezi wao Vilevile, amewataka pia wanafunzi wasome kwa bidii na kufaulu masomo yao, ambapo Serikali imeendelea kuwajengea miundo mbinu imara ya Shule, na mwaka huu Rais Samia ameshatoa tena fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za Sekondari.

Shule ambazo zimefaidika na mgao wa taulo hizo za kike ni shule zilizoko katika pembezoni mwa wilaya ya Lushoto ambapo ni shule mbili za Sekondari ambazo ni Prince Claude na Ubiri Sekondari ambapo Shule za msingi ni Bombo na Nyankei.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...